Na Chande Abdallah UKISIKIA simulizi ya Hafsa Ramadhani (19) itakutia simanzi, itakutesa moyo na kukutoa machozi, huwezi kuamini aliingia kwenye ndoa bila kujua kuwa alikuwa akienda kukutana na ugonjwa wa ukimwi, Risasi Mchanganyiko linakufunulia. Habari kutoka chanzo chetu cha kuaminika zinasema, binti huyo alifanyiwa mipango ya ndoa bila yeye na mumewe huyo kupima kwanza maambukizi ya ugonjwa huo, ingawa tahadhari hiyo ilitolewa mapema kwa kuwa muoaji alikuwa akijulikana kuwa aliishi na ugonjwa huo kwa muda mrefu. ILIKUWAJE? “Huyo binti alitokea Bukoba, akaja hapa Dar es Salaam kutafuta kazi. Akaanza kufanya kazi za ndani, akiwa mdogo kabisa. Alihangaika kwenye nyumba mbalimbali lakini baadaye akafikia kwenye kituo cha watoto yatima (kwa sasa tunahifadhi jina), kipo Charambe ambapo alianza kuishi hapo,” kilipasha chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini. “Alipofikisha umri wa miaka 15 tu, wale watu wa pale kituoni wakamu...