KUTOKA KWA JOYCE KIRIA: UNGEKUWA NI WEWE AU NI MWANAO KANG'ATWA NA KUHARIBIWA HIVI UNGEJISKIAJE
Leo tutakuletea mwendelezo wa ukatili kwa kina, aliyokuwa akiupata binti Yusta kwa mwajiri wake kung'atwa mwili mzima.. Yusta amepata mateso makali sana kwa miaka minne mfululizo na kuambulia madhara makubwa sana kwenye mwili wake ambao umepoteza unadhifu kutokana na majeraha meeeengiiiii sana.. Bi,Modesta Saimon ni mama mzazi wa Yusta akielezea jinsi alivyo umizwa na tukio. Ni dhahiri shairi kwamba mama huyu amebeba maumivu ya wakina mama wanaotuma watoto wao kuja kufanya kazi na kuambulia mateso yasiyoelezeka. Cha kusikitisha Yusta amefanyiwa unyama huo na Mwanamke! Mama! Msomi! Anajulikana kwa jina la Amina Maige... Huyo ndo mwanamke aliyefanya Unyama huo Amina Maige. Kina mama jamani tuache roho mbaya.. huyu mama ana mtoto wake wa kike.... Mtoto wa mwenzio umtafune namna hii kweli??? Ulemavu huu wa makusudi jamani kwa Mungu tutajibu nini?????? Ee Mungu turehe...