HIZI NDIZO NJIA NA NAMNA YA KUMFANYIA MUMEO AWAHI NYUMBANI!
SIPENDI na wala sitaki kusikia kwani inamkoseshe raha mtoto wa mwenzio, kuku wako mwenyewe kwa nini akushikie manati. Kwa nini uishi na mumeo kama kaka yako? Sipendi na kama unatabia hizi ukome na ukomae. Ooh! Samahani hata salamu nimesahau kukujilieni hali wote wapenzi wa kona hii najua akina mama pekee hata kina baba kuna mtu mzima mmoja aliniambia akikosa kusoma kona hii hujisikia mgonjwa kwa vile amepata mengi kupitia hapa. Haya tuendelee na yetu hasa yaliyonifanya nifungue mdomo wangu. Kuna baadhi ya wanawake wenzangu wananiudhi sana kufikia hatua ya kukosa raha, unamuonea haya mumeo au mpenzio mkiwa ndani full khanga sipendi eeeh! Umesikia mwili wako mkiwa faragha si mali yako bali ya mwenzako. Unauficha una kasoro gani mwenzio anahitaji kuliona umbile lililomvutia likiwa na nguo ameliweka ndani ili alifaidi kwa kuliona live, wewe na mikhanga kutwa kucha hata kujipaka mafuta hujipaki mbele ya mwenzio. Mumeo amekuwa akihangaika kuutazama mwili wako...