Posts

Showing posts from August 6, 2016

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 06.08.2016

Image
Posted by JAFE MALIBENEKE at Saturday, August 06, 2016 Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Pinterest

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA KATIKA KIWANDA CHA MTIBWA SUGAR.

Image
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha sukari cha Mtibwa   kukagua uzalishaji  wa sukari katika kiwanda hicho, Agosti 2, 2016.   Kulia ni  mkewe Mary, wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe na Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha sukari cha Kagera na Mtibwa, Seif Ali Seif .  Kushoto ni Kaimu Katibu wa CCM mkoa Wa Morogoro, Kulwa Solobi.   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Meneja wa Kiwanda cha sukari cha Kagera,  Ashuwin  Rana baada ya kuwasili kwenye  kiwanda  cha sukari cha Mtibwa  baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha sukari cha Mtibwa Agosti 2, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe na wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Kagera Sugar na Mtibwa Sugar, Seif  Ali Seif .   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la mtambo wa maji ya kumwagilia katika shamba la m...

Jide, Mwarabu wazua utata

Image
STORI: MWANDISHI WETU, Risasi Jumamosi MKONGWE wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Jide’ na Mwarabu mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, wamezua utata wa aina yake kufuatia msanii huyo ‘kumposti’ mara kwa mara kwenye mtandao wake wa Instagram. Risasi Jumamosi lilianza kumfuatilia Jide baada ya kutonywa na chanzo kuwa msanii huyo amekuwa akimposti Mwarabu huyo na kwamba kuna kila dalili ni mtu wake aliyerithi mikoba ya aliyekuwa mumewe, Gardner Habash.   “Nyie kama vipi fuatilieni kwa makini kwenye Instagram yake, mtagundua tu ukweli, kuna kitu maana hata akimposti huyo jamaa huwa anaweka maneno yenye utata, hataki kufunguka moja kwa moja kama ni mpenzi wake au vipi,” kilisema chanzo hicho. Baada ya chanzo hicho kulitonya Risasi Jumamosi, mwanahabari wetu aliingia kwenye ukurasa wa Jide na kuziona picha tofauti zikimuonesha akiwa amekaa na Mwarabu huyo huku akisindikiza na ujumbe ambao hautoi majibu ya moja kwa moja kama ni mtu wake au la. ...

RC MAKONDA AKUTANA NA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA (FFU) UKONGA JIJINI DAR LEO

Image
-Awapongeza kwa Uzalendo wao Kwa Taifa letu . -Awaahidi kuwapatia Ambulance  -Awataka Waifanye Dar Kama Dubai Kiulinzi.  Mkuu wa Mkoa wa Dar Mh.Paul Makonda Leo amekutana na kikosi cha kutuliza ghasia(FFU)ukonga Jijini Dar na amezungumza mengi moja kubwa nao ni Mhe. Makonda amewaeleza kuwa hakuna wafanyakazi wazalendo kama Askari kwani wao wako tayari kufa ili taifa letu Liwe salama. Makonda aliongezea kwakusema uzalendo wao hauko kwenye mshahara bali utaifa kwani hakuna mshahara unaoweza kununua uhai wa mtu.Rc Makonda amewaahidi kuendelea kuwa pamoja nao na kuwaomba wafanye dar iwe kama dubai ambapo mtu anaweza kuacha mzigo wake na kesho akaukuta. Rc.Makonda anaamini dar inapaswa kuwa salama zaidi ili watu wafanye kazi bila hofu na hata majumba yasiwekewe mageti endapo tu usalama utakuwa mkubwa.  Mwisho Mh.Makonda amewahakikishia askari hao wa FFU ukonga kuwapatia gari la wagonjwa ili liwasaidie askari katika hospitali yao huku akiahidi kufatili...