Posts

Showing posts from March 14, 2015

SIMBA SC WAICHAPA MTIBWA SUGAR BAO 1-0 TAIFA,OKWI AWAPA RAHA

Image
Wachezaji wa Simba SC wakimpongeza Okwi leo baada ya kufunga bao pekee la ushindi dakika za lala salama dhidi ya Mtibwa Sugar Na Mahmoud Zubeiry BAO la Emmanuel Anord Okwi dakika ya 90 ushei limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Simba SC sasa inafikisha pointi 29 baada ya mechi 18 na kuendelea kukamata nafasi ya tatu, nyuma ya mabingwa watetezi, Azam FC pointi 30 za mechi 16 sawa na vinara Yanga SC, wenye pointi 31. Okwi alifunga bao hilo, wakati tayari baadhi ya wapenzi wa Simba SC wameanza kutoka uwanjani, wakiamni matokeo ni sare.  Mganda huyo, alifunga baada ya kupata pasi ya Abdi Banda na kumchambua vizuri kipa aliyefanya kazi nzuri leo, Said Mohamed Kasarama. Emmenuel Okwi akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Said Mkopi katika mchezo wa leo Beki wa Simba SC, Hassan Kessy akimtoka kiungo wa Mtibwa Sugar, Shaaban Nditi...

HAPENDWI MTU INAPENDWA POCHI...JANGA LINALOVUNJA NDOA!

Image
NImatumaini yangu wapenzi wasomaji wa safu hii mko poa na mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Tumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufika siku ya leo na kuweza kuperuzi ukurasa huu muhimu wa kuzungumzia masuala ya uhusiano. Leo napenda nizungumze nanyi kuhusu mada iliyopo hapo juu. Kwa uchunguzi mdogo nilioufanya, inaonekana ndoa zilizofungwa miaka ya 80 kurudi nyuma zilikuwa na uhai mrefu kuliko miaka ya juu ya hapo. Ndoa miaka ya hivi karibuni zimekuwa zikisuasua, hazina umri mrefu. Watu wanaingia kwenye ndoa kwa kufuata kitu flani mbele ya safari kikitoweka, hayupo tayari kuvumilia, unakuwa ugomvi na ndoa kuvunjika. Wazee wetu walifunga ndoa kwa kufuata misingi ya ndoa. Kigezo cha fedha hakikupewa nafasi kubwa katika mapenzi, walitazama zaidi suala la maisha ya kusaidiana na matakwa ya Mungu katika sheria za ndoa. Mume alijua wajibu wake kama baba wa familia lakini mke pia alijua wajibu wake ndani ya familia. Kila mmoja alifuata kiapo alichokula siku ya ndo...

THIS IS WHAT THE MOST CONTROVERSIAL COUPLE IN EAST AFRICA,ZARI AND DIAMOND WILL BE DOING IN KENYA

Image
After making their relationship public and official, Zari and Diamond have been the trending topic on most social media platforms. Their 15 year age difference and the fact that Zari is currently heavy with diamond’s child has made their story even more intriguing. Amazingly, they have managed to silence their critics, their relationship has continued to flourish though many had predicted it was a passing fling. The couple is expected to jet into the country soon to attend the Art of Luxury event that will be hosted by Zari and Huddah Monroe on the 21st of March 2015. Diamond will be performing at the event and a number of DJ’s including DJ Namonsky, DJ Crème de la Crème, DJ Pierra and DJ Incredible will be show casting at the event which will be held at the Skyluxx lounge. Can’t wait to see how everything will goes down.

ANGALIA JINSI ZITTO ALIVYOITEKA KIGOMA,MAPOKEZI YAKE YASHTUA WENGI

Image
Mh zitto kabwe baada ya chama chake cha CHADEMA kutangaza kumfukuza uanachama ndani ya chama hicho ameamua kufanya ziara ya siku tatu ndani ya kigoma kuzumgumza na wananchi wake juu ya hali ya kisiasa inayomkabili kwa sasa,hizi hapa ni baadhi picha za mapokezi yake kigoma  Ikiwa bado sakata la kufukuzwa uanachama kwa mbunge wa kigoma kaskazini (CHADEMA) mh ZITTO KABWE linaendelea kuchukua nafasi katika vichwa vya watanzania na wapenda siasa,mbunge huyo ameanza kufanya ziara ya siku tatu jimboni kwake kuzungumza na watanzania mbalimbali. Akiwa katika ziara yake MBUNGE wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe(Chadema),amewataka wakazi wa mkoa wa kigoma wasisikitishwe na mambo yanayomkabili kwa sasa kwa kile alichoeleza kuwa asilimia kubwa ya wanasiasa makini walishapitia misuko suko kama yake. Amewaeleza kuwa jambo la msingi ni kumuunga mkono katika hatua yoyote atakayochukua kwa ajili ya wanakigoma na Taifa kwa ujumla katika kumaliza mgogoro uliopo...

WEMA: MUME WA ZARI ANATAKA KUNIOA

Image
MAMBO hadharani! Supastaa wa Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ ameanika siri zilizojificha nyuma ya pazia kati yake na aliyekuwa mume wa mwanamuziki nyota wa Uganda, Zarina Hassan ‘Zari’, Ivan Semwanga, kuwa anataka kumuoa, Risasi Jumamosi lina full stori. Supastaa wa Bongo Movie, Wema Sepetu ‘madam’. WALIANZIA KUKUTANA SAUZ Katika mazungumzo yake exclusive na mwanahabari wetu juzi jijini Dar, Wema alianza kwa kuweka bayana kwamba, mawasiliano yake na Ivan yalianzia nchini Afrika Kusini wakati alipokwenda kikazi, Februari, mwaka huu. “Nilikwenda na Ommy Dimpoz (Faraj Nyembo). Tulikuwa na project yake lakini tulipokuwa kule, Ivan na marafiki zake walisikia kuwa mimi nipo, wakatuomba sana kupitia kwa wenyeji wetu kuwa wanataka kutuona na kutoka nao out pamoja.” ALIBANA, AKALEGEZA “Mimi nilikuwa bize sana na kazi zangu, awali niliwaambia kuwa hatutaweza lakini baadaye walitubahatisha klabu, wakaomba kukaa na sisi, mwish...

KISA BWANA, PENNY ADAIWA KUNYWA SUMU

Image
Stori: MWANDISHI WETU/Risasi MTANGAZAJI maarufu Bongo na aliyekuwa mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amedaiwa kunywa sumu kufuatia kunyang’anywa bwana na shosti yake aliyefahamika kwa jina la Diana. Mtangazaji maarufu Bongo na aliyekuwa mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’. Kwa mujibu wa chanzo, Penny na Diana walikuwa marafiki lakini wakatofautiana baada ya Diana kumteka akili mwanaume wa rafiki yake huyo na kumkoleza mapenzi hadi kufikia hatua ya kumtangazia ndoa. “Diana kampagawisha mwanaume wa watu, jamaa akatangaza ndoa na hivi ninavyokwambia siku siyo nyingi Diana anaolewa hicho ndicho kikasababisha Penny apandwe na presha hadi kufikia hatua ya kunywa sumu, alikimbizwa hospitali, akalazwa lakini sasa ametoka anaendelea vizuri,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Penny ili kujua anazungumziaje habari hizo za kunywa sumu hadi kulazwa hospitali ambapo alikanusha mad...