Posts

Showing posts from September 15, 2015

LINNAH ATUPIA PICHA MATATA

Image
  Linnah with Mbasha and Mr Blue!!

JK AMTAJA MUHUSIKA WA RICHMOND.

Image
 Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani. Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond. “Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete. Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni. Akifungua jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji. Kadhalika, Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini. Richmond Suala la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa baada ya Waziri ...

John Mnyika amtetea vikali Dr.Slaa Adai Yaliyotokea ni Kama Samsoni kwa Delila

Image
Mnyika amemtetea vikali Dr.Slaa na kupingana na wale wanaomkejeli na kumuona hana mchango CHADEMA. Mnyika anasema Dr.Slaa anao mchango wake na yaliyomkuta ni mambo kama yaliyowahi kumkuta Samsoni kwa Delila. Naomba kuisha hapa.

LOWASSA AENDELEA NA KAMPENI ZA KUSAKA URAIS SHINYANGA

Image
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiongozana na aliekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Ndg. Hamis Mngeja wakiwapungia wananchi wa Mji wa Kahama, wakati wakiwasili kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI . Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokelewa na Mwenyeji wake, Mgombea Ubunge wa Ukawa kupitia CHADEMA, Mh. James Lembeli, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo. Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akilakiwa na maelfu ya wakazi wa mji wa Kahama, leo Septemba 14, 2015. Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Ch...

MAGUFULI ALIVYOTIKISA MJINI TABORA LEO

Image
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,akiwahutubia Wananchi wa Tabora jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa  Ali Hassan Mwinyi.Dkt Magufuli alisema kuwa Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote.  PICHA NA MICHUZI JR-TABORA  Sehemu ya umati wa watu waliokuwa katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo walipokuwa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli.    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa tabora mjini na kuwaambia kuwa Dk. Magufuli ni kiongozi sahihi anayehitajika Tanzania kwa sasa na kuwataka wananchi kumpigia kura zote ifikapo Oktoba 25...