Diamond uso kwa uso na Rich Mavoko
Diamond wamekutana na Mavoko katika ofisi hizo kwa lengo la kuongelea tofauti zao ambazo zimejitokeza kwa kile kinachodaiwa kuwa Rich Mavoko amejitoa katika lebo hiyo.
Mavoko alijiunga na WCB mwaka 2016 akisaini chini ya lebo hiyo na kuanza kufanya kazi akiwa chini ya lebo hiyo ambayo boss wake ni Diamond Platinumz.
Baada ya kujiunga na lebo hiyo Mavoko alianza malalamiko mapema mwaka huu kuwa anataka kujitoa katika lebo hiyo ya WCB wasafi kwa madai kwamba ananyonywa kimaslahi.
Mbali na kunyonywa kimaslahi lakini pia ilidaiwa kuwa kuna vitu ndani ya makataba huo msanii huyo hakutimiziwa na boss wake kama mkataba ulikuwa unaelekeza.
Malalamiko ya Mavoko yalionekana kuwagusa wengi na ikachangia Mavoko kukaa kimya kwa muda ingawa siku za hivi karibuni aliachia ngama yake mpya inayokwenda kwa jina la Ndegele.
Katika moja ya mahojiano aliyofanya meneja wa Diamond Salam Sk katika moja ya Redio hapa nchini alipoulizwa kuhusiana na madai haya ya mavoko alisema “Mavoko bado ni msanii wa WCB na hayo malalamiko anayotoa sisi hatujui yanahusiana na nini kwani huduma zote wanazopatiwa wasanii wa WCB anazipata”
Meneja huyo aliongeza “Kabla ya mavokonkusaini mkataba alipewa akakae nao aupitie hadi ajirizishe na Mavoko alifanya hivyo na kukaa nao ndani ya wiki mbili ndio akaurizia mwisho wa siku akaja kusaini sasa anacholalamika ni nini? sisi hatujui kwani makataba huo una kurasa 10 kwahiyo hatujui ni kitu gani anataka haswa”
Baada ya Mavoko kupeleka malalamiko hayo Basata,Basata nao waliamua kuwaita Maboss wa WCB walipofika wakaongea nao na ndio wakakubaliana wakutane siku ya leo August 23 katika ofisi hizo hapa Jijini Dar Es Salaam.
Mavoko amefanikiwa kutoa ngoma kadhaa akiwa chini ya lebo hiyo ya Muziki Tanzania na baadhi ya ngoma alizotoa ni pamoja na “Imabaki stori,Kokoro akishirikiana na Boss wake Diamond,Show me akishirikiana na Harminize pamoja na Rudi akifanya na msanii kutoka Nigeria Patoranking.
Comments
Post a Comment