Posts

Showing posts from October 18, 2016

Khadija Kopa Kuwasha Moto Krismas Morogoro

Image
Mwenyekiti na mratibu wa tamasha hilo, Hamis Abdallah,  akizungumza jambo na wanahari (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni mkuu wa matukio kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kurugira Maregesi,  Hamis Abdallah na Khadija Kopa. Khadija Kopa akizungumza jambo. Kiongozi wa FM Academia, Nyoshi El Saadat, akielezea namna atakavyopagawisha mashabiki wake. MALKIA wa muziki wa taarab ambaye ni Mkurugenzi wa Kundi la Ogopa Kopa, Khadija Kopa,  anatarajiwa kuwasha moto kwa kutoa burudani ya aina yake katika  Tamasha la Muziki wa Taarab  lililoandaliwa na mtandao wa habari wa Vijana, Tegemeo Arts Group ambalo linajulikana kwa jina la ‘Nani Zaidi’. Tamasha hilo litakaofanyika siku ya X-Mass ya Desemba 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi usiku. Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, mwenyekiti na mratibu wa tamasha hilo, Hamis Abdallah,  amesema tamsha hilo linalenga kuh...

Rais JPM Atengua Uteuzi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Tanga

Image
Rais Dk. John Pombe Magufuli. Rais Dk. John Pombe Magufuli leo ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, Emmanuel Mkumbo. Bwana Mkumbo alikuwa anakabiliwa na tuhuma za kujifanya ofisa wa usalama wa taifa nakumtishia kwa bastola askari wa usalama barabarani wakati wakielekea kituo kidogo cha polisi Kingoluwira, Morogoro alikotaka apelekwe kuzungumza na mkuu wa kituo baada ya kukamatwa akiwa amezidisha Mwendo kasi katika barabara kuu ya Morogoro – Dar es Salaam.

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA MAELFU KUAGA MWILI WA MEYA WA ZAMANI WA DAR ES SALAAM DKT. DIDAS MASABURI

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea machache kwenye hafla ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016.  Sehemu ya wafiwa kwenye hafla ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masa b uri katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe wakitoa heshima zao za mwisho na kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe wakiwapa pole wafiwa baada ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ...