Zombe na Wenzake Washinda Kesi, Christopher Bageni Kunyongwa
Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kinondoni, SP Christopher Bageni (kushoto) baada ya kuhukumiwa kunyongwa akiagana na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Abdallah Zombe (katikati). …Akiongea jambo na aliyekuwa wakili wake baada ya hukumu kutolewa. Polisi wakimpeleka katika chumba maalum mahakamani baada ya hukumu kutolewa. Bageni akielekea katika chumba maalum. Abdallah Zombe (mwenye nguo nyeupe katikati) akiwa na ndugu zake baada ya kuachiwa huru. BAADA ya kimya kirefu, Mahakama ya Rufaa leo imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Abdallah Zombe, na maofisa wenzake wawili. Hata hivyo, mahakama hiyo imemuhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kinondoni, SP Christopher Bageni. Zombe na wenzake walikuwa wakituhumiwa kuwaua wafanyabiashara watatu wa...