Ufisadi Mkubwa Wizara ya Afya Wagundulika..Wakati Watoto Wakikosa Chanjo Mahospitalini..Hivi Ndivyo Mabilioni ya Pesa Yalivyotafunwa na Wajanja Wachache..!!!
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mwaka wa fedha 2015/16 imebaini ufisadi wa mabilioni ya fedha katika mradi wa chanjo ya Surua Rubella na ameshauri kufanyika uchunguzi wa kijinai na waliohusika warejeshe fedha hizo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hayo yalibainika wakati wa ukaguzi maalumu katika halmashauri za wilaya na ofisi za waganga wakuu wa mikoa. Ukaguzi huo umebaini Sh20.9 bilioni zilipokelewa na Wizara ya Fedha kutoka Gavi Alliance na kiwango hicho chote kilipelekwa Wizara ya Afya kugharamia chanjo ya Surua Rubella. Kati ya kiwango hicho, Sh19.09 bilioni zilitolewa kwa ajili ya chanjo; Sh18.3 bilioni zilitumika Tanzania Bara na Sh725 milioni zilipelekwa Zanzibar na Sh1 bilioni zilitumika kama gharama za uendeshaji. Ripoti hiyo imeainisha kuwa hadi Desemba 31, 2014 kulikuwa na bakaa ya Sh838,423,408. Fedha zilizopokelewa halmashauri Ripoti hiyo inaainisha kuwa Sh17.3 bilioni zilitumwa katika mikoa na kuing...