BREAKING NEWS: MASIKINI WALE WATOTO MAPACHA WA KIKE WALIOZALIWA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MARA WALIOUNGANA KIFUA WAMEFARIKI DUNIA,MWANZA
Watoto mapacha wa kike waliozaliwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara iliyopo mjini Musoma wakiwa wameungana sehemu ya kifua na tumbo wamefariki dunia jana majira ya saa 9.10 alasiri wakiwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza kabla ya kufanyiwa upasuaji. Watoto hao pacha walizaliwa januari 4 mwaka huu na mama mmoja mkazi wa manispaa ya Musoma Helena Paulo wakiwa na uzito wa kilo 4.6 na kisha kusafirishwa hadi katika hospitali ya rufaa Bugando kwa ajili ya uchunguzi zaidi ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha. Dk. Shukuru Kibwana ambaye ni daktari katika wodi ya watoto ya hospitali ya rufaa Bugando, amesema timu ya madaktari wa upasuaji na wataalamu wengine wamefanya kila lililowezekana kuokoa maisha ya pacha hao walioungana lakini haikuwezekana na kuongeza kuwa kabla ya upasuaji, mapacha hao walitakiwa kupitia tomografia ( CT ) na kufanya kipimo cha ultra sound ili kujua kama watoto hao wameungana ...