JINSI YA KUPUNGUZA ULAJI SUKARI
Ulaji wa sukari kupita kiasi unahusishwa na kuongezeka kwa unene, uzito kupita kiasi, ugonjwa wa kisukari cha ukubwani (aina ya pili), magonjwa ya moyo, baadhi ya saratani, kuoza kwa meno na ugonjwa wa ini. Katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, siyo rahisi kufanya tafiti zinazoonyesha kiasi cha sukari anacho kula mtu kwa siku. Kwa hiyo, hatuna budi kutumia takwimu za nchi zilizoendelea kama Marekani na ulaji wa watu wake haupishani sana na baadhi ya Watanzania wanaoishi mijini. Baadhi ya tafiti za miaka ya 2008-2009 zinaonyesha kuwa nchini Marekani mtu mzima kwa wastani anakula sukari vijiko vya chai 22 kutoka katika vyakula vilivyosindikwa kiwandani. Kwa mujibu wa Taasisi ya Kimarekani ya Mambo ya Moyo (Aha), kwa watu wazima, wanawake, matumizi yao ya sukari inayotokana na vyakula vilivyosindikwa kiwandani, yasizidi vijiko sita vya chai kwa siku. Kwa wanaume wasizidishe vijiko tisa kwa siku. Watu wafahamu kila gramu nne za sukari ni sawa na sukari iliyojaa kati...