Posts

Showing posts from December 2, 2016

Ndege mpya ya ATCL yapata hitilafu uwanja wa ndege Arusha

Image
Ndege mpya ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) jana ilipata hitilafu katika uwanja wa ndege wa jijini Arusha hali iliyopelekea ndege hiyo kushindwa kuendelea na ratiba kama ilivyokuwa imepangwa. Taarifa kutoka katika uwanja wa ndege wa Arusha zinaeleza kuwa tairi moja ya ndege hiyo lilipata pancha ikiwa katika barabara ya kurukia ndege. Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo alisema kuwa tairi moja ya ndege hiyo lilitoka nje ya barabara ya ndege kukimbilia wakati ndege hiyo ilipokuwa inatua uwanjani hapo hivyo ikakwama kwenye nyasi. Chanzo cha ndege hiyo kutoka nje ya barabara ya kukimbilia ndege kimeelezwa kuwa ni wembamba wa barabara hiyo kiasi kwamba rubani akikosea kidogo tu, basi ndege hutoka nje. Hadi sasa Shirika la Ndege la Tanzania halijatoa taarifa yoyote kuelezea tukio hilo.