Posts

Showing posts from March 10, 2016

RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongeza na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea jambo na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu alipokutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kukutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza

RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA GHAFLA BENKI KUU (BOT) JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Naibu Gavana wa BOT Dkt. Natu Mwamba akiwasili makao  makuu ya Benki Kuu ya Tanzania alikofanya ziara ya kushtukiza leo Machi 10, 2016 .

DK.KIGWANGALLA AKUTANA NA MADAKTARI WALIOHITIMU MAFUNZO KWA VITENDO 2014/15

Image
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akifuatilia mkutano huo uliowakutanisha Madaktari waliohitimu mafunzo kwa vitendo 2014/2015 (waliokaa upande wa kushoto). Wengine waliokaa upande wa kulia ni viongozi watendaji wa ngazi za juu wa Wizara hiyo wakifuatilia mkutano huo. Madaktari hao walifanya mkutano huo kwa lengo la kutaka kufahamu masuala mbalimbali ikiwemo suala la ajira. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kutoka kushoto) akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi hao juu ya mipango ya Wizara hiyo na namna ilivyojipanga ikiwemo kushughulikia suala lao hilo ambalo ni la kiutawala zaidi.

MASANJA Atoa SIRI ya Utajiri Wake... Atoa Somo Zito Kwa Vijana Wa Mjini Wanaopenda Mteremko!

Image
  Laki tano, Mshahara wa Ma-Teller wa Benki hapa mjini Laki Tano, Bei ya TECNO PHANTOM mpya kabisa kwa kujishau Snapchat na Istagram Laki Tano, Bajeti ya Mafuta ya SUBARU mwezi Mzima.... Laki Tano , Bajeti ya HEINEKEN 100 KWA wanywaji wa Pombe... HELA FLANI MBUZI TU ambayo wengi wanaona HAINA ISHU .   Lakini , Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji.   Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua SIMTANK la lita 5000 ( ndoo 250 za lita 20) ambal inaweza kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila SIMTANK unalouza.   Laki tano hii hii inaweza kulima Ekari 2 za Maharage pale Simanjiro na baada ya Miezi Minne ukavuna si chini ya Million 3 ambazo zitaexpand kilimo chako MARA 6 zaidi ya Mwanzo na Kuexpand Kipato chako mara 6 zaidi ya Mkupuo wa kwanza!   Laki Tano hii ina uwezo wa kulima Matikiti Maji Ekari 2 n

Diamond, Tiffah Wapima Sauzi

Image
Mtoto Latifah Nasbu ‘Tiffah Musa Mateja, AMANI DAR ES SALAAM! Hii ni EXCLUSIVE stori! Kufuatia kelele kibao kutoka kwa wadau mbalimbali kwamba mtoto wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, yaani Latifah ‘Tiffah’ aliyemzaa na Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ si wa nyota huyo, hatimaye, jamaa ameamua kupima vinasaba ‘DNA’ (DeoxyriboNucleic Acid). ISHU ILIKUWA AFRIKA KUSINI Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, Diamond aliamua kutekeleza mpango huo nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ ambako aliamini hakuna ‘macho mengi’ ya watu, hususan mapaparazi. Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ SIKIA HII “Jamani mimi nataka niwape stori ambayo ni ya uhakika. Hivi mnajua kwamba Diamond aliamua kwenda Sauzi kupima DNA yake na mtoto wake Tiffah? “Kutokana na manenomaneno ya watu, ilifika mahali alichoka, akawa njia panda. Hivyo ili kuondoa figisufigisu, akamwambia Zari waende wakampime DNA mtoto na yeye. Ni kabla hajaenda Marekani.” MAJIBU HAYA HAPA Chanzo hicho kikas

RAIS WA ZANZIBAR AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA VIETNUM, AKUTANA NA MAALIM SEIF

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, jana Ikulu Jijini Dar es Salaam akipofika kwa mazungumzo na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Ujumbe wake (kushoto) wakiwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Rais wa Vietnam Truong Tan Sang jana Ikulu Jijini Dar es Salaam akiwa nchini kwa ziara ya Kikazi,[Picha na Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akiagana na mgeni wake Rais wa Vietnam Truong Tan Sang(kushoto) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam(katikati) mawair mbali mbali wa Vietnum walioungana na Rais  Truong ,[Picha na Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akifuatana na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang(katikati) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Sala

Rais wa Zanzibar Dr. SHEIN Amtembelea na Kumjulia hali Maalim SEIF Jijini Dar es Salaam

Image
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiambatana na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala bora Mheshimiwa Dkt. Mwinyihaji Makame, amemtembelea kumjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad ambaye yuko hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko baada ya kutolewa hospitali. Amesema afya yake inazidi kuimarika siku hadi siku. Dkt. Shein alifika hotelini hapo jana saa mbili usiku. (Picha na Salmin Said, OMKR)     Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akimjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanibar Maalim Seif Shariff Hamad hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam       Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akimjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanibar Maalim Seif Shariff Hamad hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Picha na OMKR

Tumekwishaa! Poda Zadaiwa Kusababisha Kansa

Image
Boniphace Ngumije na Gladness Mallya, RISASI Mchanganyiko DAR ES SALAAM: Kuna neno moja tu linaloweza kusemwa kwa sasa, kuwa tumekwisha, baada ya kubainika kuwa poda iliyotumika kwa miaka mingi nchini, ambayo ni maarufu kama Johnson’s Baby Powder inadaiwa kusababisha kansa ya kizazi inayoleta maafa ikiwemo vifo. Taarifa zilizopatikana kupitia mitandao ya internet, zinadai kwamba kampuni inayotengeneza poda hiyo ya Johnson and Johnson ya Marekani, Februari 25, mwaka huu ilihukumiwa kulipa faini ya kiasi cha dola milioni 72 (sawa na shilingi bilioni 144) katika Mahakama ya Missouri kama fidia kwa mwanamke mmoja aliyefariki dunia kwa kansa ya kizazi iliyotokana na matumizi ya vipodozi hivyo. Familia ya mwanamke huyo, Jacqueline Fox ilitakiwa kulipwa kiasi hicho cha fedha baada ya mahakama kuridhika kuwa ugonjwa na kifo chake kilitokana na matumizi ya vipodozi hivyo kwa zaidi ya miaka 35, akitumia poda pamoja na losheni ya bidhaa hiyo. Kampuni hiyo ya Johnson &

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 10.03.2016

Image