POLISI FEKI 7 WANASWA TENA....
SIKU chache baada ya kukamatwa kwa askari feki wa usalama barabarani, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imewakamata watuhumiwa saba wa ujambazi, wakiwa na sare za Polisi, huku mwingine akijifanya ofisa Usalama wa Taifa. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaa, Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na sare za Polisi jozi mbili. Watuhumiwa hao ni Khamis Mkalikwa (40), Magila Werema (31), Nurdin Bakari (46), Materu Marko (32), Louis Magoda (34), Amos Enock (23) na Amiri Mohammed (45), wote wakazi wa jijini Dar es Salaam. Sare hizo, kwa mujibu wa Kamanda Kova, ni zenye cheo cha Sajenti wa Kituo, huku jozi moja ikiwa na jina linalosomeka SSGT A.M Mduvike. Watuhumiwa hao walikamatwa jana katika eneo la Kiluvya, baada ya askari kuweka mtego, ambao ulifanikiwa kuwanasa. Alisema watu hao walikuwa wakitumia silaha, sare za jeshi la Polisi na redio ya m...