Posts

Showing posts from February 24, 2016

Mnaotarajia Kuoa au Kuolewa Chukueni Tahadhari Hii Mapema Usijejuta.....

Image
Ewe mwanaume ukioa mwanamke: Mrefu, jua kwamba utaoa mwanamke mpenda maendeleo, mchapa kazi na mkarimu ila hawajui mapenzi na ni wavivu kujiweka safi kimazingira. Mfupi kiasi , jua ya kwamba utaoa mwanamke mchangamfu na mpenda elimu sana ila tu wanapenda mnongono na hawaridhiki. Mfupi kabisa. Jua ya kwamba utaoa mwanamke msikivu na mcha Mungu ila ni waroho kwa kula na wabishi sana. Ewe mwanamke ukiolewa na mwanaume: Mrefu, jua ya kwamba utaolewa na mwanaume mwenye upendo, utu na ubinadamu ila ni wabahili mno na hawapendi kupendeza. Mfupi kiasi, jua ya kwamba utaolewa na mwanaume mwenye fikra na akili timamu za maendeleo, mbunifu, mcheshi na fundi wa mahaba ila ni wapenda ushirikina sana, wana wivu na wambea sana na mara nyingi hupenda kupiga chabo kwa watu wanaofanya mapenzi. Mfupi kabisa, jua ya kwamba utaolewa na mwanaume mwaminifu, msikivu, mnyenyekevu ila huwa wepesi wa kujiua, kukata tamaa upesi, wanawivu sana na hawapendi kuoga. Nawa...

Malalamiko ya Mikopo Elimu ya Juu Yapatiwa Ufumbuzi

Image
Kutoka kushoto ni Ofisa Habari Mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Veneranda Malima,Meneja Habari Elimu na Mawasiliano,Omega Ugole na Mkurugenzi Msaidizi wa Utoaji Mikopo, Elias John. Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

Hizi hapa ni picha za Obama akifurahi na watoto ambazo zimegusa hisia za wengi

Image
Rais wa Marekani , Barack   Obama ni miongoni mwa watu wanao pendwa, huu ni uthibitisho ambao wengi wanaweza kukubaliana nao. Katika mafanikio yake katika siasa na ukaribu na watu umemfanya watu wengi wawe wanampenda lakini kupitia picha hizi akiwa na watoto zimegusa hisia zaidi. Obama hajawahi kuwa mtu wa kuzuia hisia zake, Kama akifikwa na machozi basi hata mbele za watu hutokwa na machozi, Picha hizi zilizo wekwa mandaoni zikiwa na hashtag #ObamaAndKids zimeonyesha hisia zake kwa watoto. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

MAMBO YAWA MAGUMU KWA WAZIRI WA ZAMANI WA CCM MAIGE NAE ATAJWA UFISADI NGORONGORO

Image
Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii katika serikali ya awamu ya nne, Ezekiel Maige, jana alitajwa katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Bernard Murunya  ambaye ameshitakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi. Katika kesi hiyo, Maige anadaiwa kulipiwa nauli ya safari ya nje na mamlaka hiyo kwa idhini ya Murunya, ambaye sasa ni Mbunge wa Afrika Mashariki.  Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, Sezari Semfukwe, alidai kuwa Murunya na aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mamlaka hiyo, Shad Kiambile, waliidhinisha malipo ya dola 66,890. Alidai kuwa fedha hizo zilikuwa kwa ajili ya safari ya Maige na msaidizi wake aliyetajwa kwa jina la E. Muyungi na Murunya mwenyewe. Semfukwe, ambaye ni Kaimu Mhasibu Mkuu wa mamlaka hiyo, alidai kuwa Murunya na Kiambile, ndio walioidhinisha madokezo kwa ajili ya malipo hayo.  Akiongozwa na Wakili wa Serikali Hamidu Sembano, akisaidiana na Rehema Mteta, mbele ya Haki...

Ndege Yapotea ikiwa na watu 23

Image
Ndege ndogo ya shirika la ndege la tara Airlines iliyokuwa na watu 23 wakiwemo watoto imepota ikiwa maeneo ya usawa wa milima Magharibi mwa Nepal. Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Pokhara, Magharibi mwa Mji Mkuu Kathmandu, kwenda Jomsom, eneo ambalo watu wengi wanaoenda kukwea milima ya Himalaya huanza safari yao ya kukwea milima hiyo. Ripoti zinasema mabaki ya ndege hiyo yamepatikana ingawa hakuna taarifa zozote kuhusu vifo au majeruhi. Taarifa zaidi zinasema kuwa, Ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na maafisa wa udhibiti wa safari za ndege wa Pokhara dakika 18 baada ya kupaa na kwamba hakuna viwanja vya ndege kati ya maeneo hayo mawili. Maafisa wanasema ndege hiyo ya shirika la Tara Airlines ilikuwa na marubani watatu na abiria 20, mmoja wao raia wa China na mwingine wa Kuwait. Wawili kati ya abiria waliokuwa wamebebwa na ndege hiyo walikuwa watoto. Tangu mwaka 1949, kumetokea zaidi ya ajali 70 zilizohusisha ndege za kawaida na helikopta, na vifo vya watu 700....