Uwoya ni Gusa Unate!
DAR ES SALAAM: Msanii maarufu wa filamu Bongo, Irene Uwoya (pichani) anatajwa kuwa kati ya mastaa wa kike Bongo aliyewahi kutoka na mastaa na vigogo mbalimbali huku ikidaiwa kuwa, kila aliyekuwa naye alimuacha yeye na si kuachwa. Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Uwoya aliyeomba hifadhi ya jila lake, staa huyo mwenye shepu na mvuto wa kudatisha kimahaba amekuwa akipapatikiwa sana na wan aume lakini mwisho wa siku huishia kuwaliza kwani yeye ndiye anayeamua kuendelea na wewe au akuache. “Uwoya namjua vizuri sana, yule ni hatari kwa wanaume. Kwanza anajijua kuwa ni mzuri hivyo amekuwa akiwadenguliwa wanaume wengi sana na orodha ya wanaomtokea kila siku ni kubwa. “Lakini akitokea kukupenda atakupenda kweli hadi unaweza kuona kero. Kwa kifupi anajua kupenda, kujali na kubembeleza kiasi kwamba ukinasa kwake ni vigumu kutoka ndiyo maana wapo wanaosema kwamba, Uwoya ni gusa unate! “Ila sasa, anaweza kukuchanganya kwa mahaba mazito lakini siku akiamua kukuacha, a...