Mzee Zahir Zorro alivyowakosha wakazi wa Mwanza
Mwanamuziki wa siku nyingi nchini kwenye muziki wa dansi na rhumba, Zahir Ally Zoro (pichani) usiku wa kuamkia Jumamosi aliwaburudisha vilivyo wakazi wa Jiji la Mwanza baada ya kufanya shoo kali katika Ukumbi wa Kilimanjaro Hotel, Nyegezi. Ilikuwa ni shoo yake ya kwanza kwa mwaka huu 2016 ambapo wapenzi wa muziki wa dansi na rhumba walivutiwa na burudani iliyotolewa na Zorro hasa baada ya kuimba live wimbo uitwao “Beatrice” ambao ni wimbo uliofanya vizuri sana wakati anauachia akiwa na bendi yake ya Mass Media. Burudani kutoka kwa Zahir Ally Zorro ikiendelea. JJ Band kutoka Jijini Mwanza, pia walifanya shoo kali katika kumsindikiza Zahir Ally Zorro. Ilikuwa Shoo kali sana ikizingatiwa kwamba wakazi wa Jiji la Mwanza huwa wanaumiss muziki wa dansi/rhumba. Twiga Band kutoka Jijini Mwanza pia walimsindikiza Mzee Zahir Ally Zorro ambapo walifanya shoo nzuri na hivyo kuonyesha kwamba kwa siku za hivi karibuni Mwanza kutakuwa na bendi nzuri. Zahir ...