Posts

Showing posts from April 10, 2018

Kufungiwa Nyimbo za Diamond Kwazua Gumzo Bungeni

Image
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kupitia Vijana Mkoa wa Arusha ,  Catherine Magige. MBUNGE wa Viti Maalum (CCM) kupitia vijana Mkoa wa Arusha, Catherine Magige amehoji kufungiwa baadhi ya nyimbo za staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, wakati kamati ya maudhui ilikuwepo na kuziacha nyimbo hizo zikaenda hewani kwa muda mrefu. Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Akijibu swali hilo, Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison  Mwakyembe,  amejibu kuwa Diamond siyo msanii wa kwanza kufungiwa nyimbo zake kwani hata wasanii wa Nigeria,  Davido na Wizkid,   wamefungiwa nyimbo  zao. Pia alimtaja mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasiaya Congo, Kofii Olomide, ambaye wimbo wake  wa Ekoti Te umefungiwa nchini humo. Pamoja na kuibuka wabunge wengi wenye kutaka kutoa taarifa na kuendelea hoja hiyo, Naibu Spika, Tulia Ackson,  hakuwapa nafasi.

Wanaume Waliotelekezewa Watoto Wajitokeza Kwa Makonda

Image
Taswira ilivyoonekana Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Baadhi ya wanawake waliotelekezewa watoto wakisubiri kusikilizwa kero zao. Baadhi ya wanaume wa waliofika ofisi ya Makonda. . ..Wakiongea na Global Tv Online. Mmoja wa wanaume waliofika ofisi za Makonda, Vedasto Mdesa,  akizungumza na Global Tv Online. Baadhi ya wanaume wa Mkoa wa Dar es Salaam leo wamejitokeza kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  baada ya kusikia tangazo kutoka kwa mkuu huyo  juu ya kufika ofisini kwake kwa malalamiko ya kutelekezewa watoto na wanawake. Wanaume hao walikuwa gumzo kwa watu wengi kwa ujasiri huo wa kufika kwa mkuu wa mkoa ili kudai haki zao baada ya kutelekezwa na wake zao. Mmoja wa wahanga hao aliyejitambulisha kwa jina la Tito Petro  alishtua wengi baada ya kutoa kauli kuwa ugonjwa wa kupooza ndiyo chanzo kikubwa cha kusambaratika kwa familia yake. Agizo hilo la wanaume kujitokeza leo, alilitoa Makonda jana baada ya siku

Wanawake waliotelekezwa wadai walizalishwa na viongozi mbalimbali

Image
WANAWAKE 480 waliotelekezwa na watoto ambao jana waliitikia wito wa kwenda kusaidiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wamesema walizalishwa na viongozi mbalimbali wa kidini na kisiasa. Hilo lilibainika baada ya wanawake hao, miongoni mwa mamia waliofika ofisini hapo  ili kupatiwa msaada wa malezi na matunzo ya watoto wao waliotelekezwa na baba zao. Katika mfululizo wa misaada ya aina hiyo, leo wanaume waliotelekezewa watoto na mama zao, watafika ofisini kwa mkuu wa mkoa huyo kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa suala hilo. Wakati huohuo, Makonda akihutubia wakati wa uzinduzi wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 unaofanyika leo katika viwanja vya Zakeem Mbagala, amesema wanawake 47 waliofika ofisini kwake jana wanadai wabunge ndiyo wamewatelekeza na watoto na wengine  wamesema  wamezalishwa na kutelekezwa na viongozi wa dini mbalimbali. Katika hafla hiyo ya utoaji wa chanjo, mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa

Basi la Kampuni ya Maqadir Lapata Ajali Tanga

Image
Muonekano wa ajali hiyo baada ya basi hilo kuanguka katikati ya barabara. Basi la Kampuni ya Maqadir lililokuwa linatoka jijini Tanga kwenda Kijiji cha Mtae, Wilaya ya Lushoto mkoani humo, limeanguka asubuhi  leo Aprili 10, 2018 katikati ya barabara kuu ya Segera-Tanga katika kijiji cha Mpakani, kata ya Kerenge wilayani Muheza mkoani Tanga. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, majeruhi wa ajali hiyo ni mmoja na bado hajatambuliwa ambapo  chanzo cha ajali hiyo, pia bado hakijafahamika.

IT SUPPORT & SYSTEMS ADMINISTRATOR

Image
Application deadline2018-04-28 Business / Employer nameResolution Insurance Company L Location Other Dar es Salaam District Dar Es Salaam Description Industry: Banking & Finance Minimum Qualification: Bachelor Minimum Experience: 2 years Reporting to the Business Analyst and IT Support and Systems Administrator’s role will be primarily accountable for the resolution of all user tickets and the maintenance of 99.9% uptime of ICT services. The main area of this roles jurisdiction is, Networks, Data centre operations, IT Support and Security. The individual will be expected to demonstrate commitment and loyalty and perform all duties in accordance with the organization’s office routines and procedures, keeping in mind the overall business objectives. Key Responsibility Areas: Responsible for the administering and ensuring high availability of Resolution Insurance corporate information systems and hardware. Administering the Resolution Insurance lo

BREAKING: MOTO WAZUA TAHARUKI BUNGENI

Image
Mwenyekiti wa bunge, Mussa Azzan ‘Zungu’ ameahirisha shughuli za bunge ikiwa ni dakika 12 kabla ya muda uliotakiwa baada ya kutokea taharuki ya moto uliosababishwa na kulipuka kwa poer bank iliyokuwa ikichaji simu ya nbubge ndani ya ukumbi wa bunge jioni hii. Aidha, mlipuko huo haujaleta madhara yoyote isipokuwa moshi mkali, hakuna aliyejeruhiwa kutokana na tukio hilo. Tukio hilo limejiri ikiwa ni muda mfupi baada wabunge wa CUF kutoka ndani ya bunge kufuatia mwenyekiti huyo kuzuia mjadala kuhusu mambo yanayohusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Waziri Mwakyembe atoa ombi hili kwa Wabunge

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amefunguka na kuwataka baadhi ya Wabunge Bungeni kuacha kuwatetea wasanii wanaoimba nyimbo zisizokuwa na maadili kwa kuwa kufanya hivyo kuna pelekea kuonekana taifa la Tanzania kuwa mfu lisilokuwa na utamaduni wake. Waziri Mwakyembe ametoa kauli hiyo leo (Aprili 10, 2018) kwenye mkutano wa 11 kikao cha sita kinachoendelea kufanyika mkoani Dodoma wakati akijibu swali la Nyongeza kutoka kwa Mbunge Catherine Magige ambaye alitaka kufahamu ni kwanini kamati ya maudhui inashindwa kufanya kazi zake kwa wakati mpaka inafikia muda wasanii wanaachia kazi zao za sanaa ndio wao wanaibuka na kuanza kuwafungia kazi hizo, je wameshindwa kazi ?. "Kila taifa lina utamaduni wake na lazima liulinde kwa udi na uvumba, tunachokifanya sisi sio kwamba tuna vita na wasanii wetu, hapana. Lakini lengo letu ni kulinda maadili ambayo katika kipindi hiki cha utandawazi kumekuwepo na mmong'onyoko mkubwa katika ta