Posts

Showing posts from June 9, 2016

Wasiotumia EFDs Marufuku Kufanya Biashara na Serikali

Image
KUANZIA Julai mosi mwaka huu, serikali imepiga marufuku kwa Wizara, Taasisi, Wakala za Serikali, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya biashara na wazabuni na wafanyabiashara wengine ambao hawatumii mashine za kielektroniki - EFDs. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema hayo jana bungeni wakati akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma jana. Aidha, Dk Mpango aliwapongeza wafanyabiashara walioitikia matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ambayo inamtaka kila mfanyabiashara isipokuwa wale ambao wametangazwa rasmi na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato kutotumia mashine za EFD kutoa risiti kila anapouza bidhaa au huduma. Alisema ili kuwa na usimamizi mzuri wa fedha za serikali na kuhakikisha kwamba zinatumika kama ilivyokusudiwa, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya Fedha za Umma na kanuni zake, alitangaza kuwa malipo yote lazima yaambatanishwe na ankara za madai au stakabadhi (tax invoice) zilizotolewa na mashin...

Huu Hapa Mchanganuo wa Bajeti ya Serikali 2016/ 2017

Image
SERIKALI imewasilisha Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 ya Sh trilioni 29.53, ambayo nguvu kubwa imewekwa katika kukusanya mapato kwa kulinda viwanda vya ndani na kubana matumizi ya serikali ili kuelekeza sehemu kubwa ya matumizi katika maeneo ya vipaumbele. Katika bajeti hiyo, bidhaa za lazima zinazogusa maisha ya wananchi ikiwemo mafuta ya petroli na dizeli pamoja na ushuru wa barabara na maji ya kunywa, havijaguswa huku bidhaa za starehe kama bia, sigara, soda, juisi na nyingine kama nguo za mitumba, huduma za kupanga nyumba na uhamishaji fedha kwa simu, vikipandishwa kodi, huku kiinua mgongo cha wabunge, kufutiwa msamaha wa kodi. Aidha, makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi, ikiwemo mapato ya taasisi za udhibiti kama Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Mafuta (EWURA), Shirika la Viwango (TBS), Jeshi la Polisi (Trafiki) na mamlaka nyingine za udhibiti, sasa yatapelekwa moja kwa moja katika Mfuko Mkuu wa Serikali ambapo mahitaji yao ya fedha yatatolewa na Wizara ya...