Posts

Showing posts from May 3, 2016

DAVID DE GEA AWEKA REKODI USIKU WA TUZO MAN UNITED

Image
David De Gea ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Manchester United kwa mara ya tatu mfululizo baada ya Jumatatu usiku kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo. De Gea ametwaa tuzo hiyo maarufu kama Matt Busby player of the year ikiwa ni baada ya kutoruhusu kufungwa bao lolote katika michezo 14 kati ya 32 ya Ligi Kuu England aliyoicheza Manchester United msimu huu wa 2015/2016 huku pia akifanya vizuri katika michuano ya kombe la FA.Mbali ya De Gea nyota mwingine aliyewahi kutwaa tuzo hiyo kubwa zaidi mara tatu lakini katika vipindi tofauti ni Mreno Cristiano Ronaldo. Ronaldo alitwaa tuzo hiyo mwaka 2004, 2007 na 2008. Akiongea baada ya kutwaa tuzo hiyo De Gea amesema: “Ni ngumu kusema chochote, kutwaa tuzo hii mara tatu mfululizo ni faraja na heshima kubwa. Napenda kuwashukuru mashabiki wetu ambao ni bora zaidi duniani”. Wengine walioshinda tuzo Jumatatu usiku ni: Chris Smalling aliyetwaa tuzo ya mchezaji

NEC YAKAMILISHA RASIMU YA KWANZA YA TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2015

Image
Kamati Maalum iliyoundwa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kuandaa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika nchini Oktoba 25, 2015 imekamilisha Rasimu ya kwanza ya Taarifa hiyo na kuiwasilisha kwa Tume. Akizungumza Katika kikao cha Tume mara baada ya kupokea Rasimu hiyo ya kwanza, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Damian Lubuva kwa niaba ya Wajumbe wa Tume amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na Kamati hiyo licha ya majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Tume hiyo kwa sasa. Jaji Lubuva ameeleza kuwa Tume imeridhishwa na kazi nzuri iliyofanywa ya kuandaa Rasimu hiyo ikiwa ni pamoja na muda mfupi uliotumika katika kukamilisha kazi hiyo. Aidha, ameongeza kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa taarifa hiyo inakamilika na kukabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema mwezi Julai mwaka huu. Pongezi hizo pia zimetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchagu

NAFASI ZA KAZI MWANANCHI MWISHO WA KUTUMA MAOMBI TAREHE 13 MAY 2016

Image
FREELANCER BUSINESS EXECUTIVE-TANGA POSITION DESCRIPTION: Mwananchi Communications Limited publishers of leading Tanzania newspapers, Mwananchi, Mwanaspoti and The Citizen are looking for motivated and highly experienced individuals to fill the positions of: – Freelancer Business Executives (16 POSTS) Dar es Salaam (8), Mtwara (1), Lindi (1), Dodoma (1), Singida (1), Zanzibar (1), Tanga (1), Kigoma(1) and Tabor(1). Job Purpose: To develop, maintain and increase a solidly dependable client base, to sell advertising space and provide an effective service to clients so as to maximise advertising sales volumes and revenue targets. . Main Responsibilities: • The successful candidates will be responsible for the following key result areas: • Thoroughly familiarizes oneself with comparative (own and competition) readership, circulation and rates and cost of advertising in all print and electronic media. • Identifies potential advertising clients, studies their bus

Aliyejifungua Watoto 3 Aomba msaada

Image
MKAZI wa Kijiji cha Mapinduzi Kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Julietha Sokoine (24) amejifungua watoto wa watatu na ameiomba serikali, taasisi,mashirika na watu binafsi kumpatia msaada wa kifedha utakaomsaidia kuwatunza watoto hao. Pia alisema msaada huo pia utamuwezesha kupata tiba ya ugonjwa wa pumu ambao umemsababisha kuvimba mwili wote. Akizungumza mwishoni mwa wiki, Sokoine ameiomba jamii kumsaidia kutokana na kukabiliwa na tatizo la ugonjwa wa pumu ambao pia umesababisha kuwa na hali ngumu ya kimaisha ambayo inamfanya kushindwa kuwatunza vizuri watoto wake. Alisema watoto hao, Daniel Sokoine,David Sokoine na Davis Sokoine walizaliwa kwa pamoja Machi 22, mwaka huu katika hospitali ya mkoa wa Dodoma huku kati ya wawili wa wakiwa na uzito kilo mbili na nusu na wa mwisho kilo mbili. “Hali yangu siyo mzuri kutokana na mimi mwenyewe kukabiliwa na tatizo la ugonjwa wa pumu,ambapo wakati mwingine nalazimika kuwanywesha maziwa ya ngombe watoto hao

Maelfu wamuaga Papa Wemba Kinshasa

Image
 Papa Wemba atazikwa Jumatano Maelfu ya waombolezaji walijitokeza kuadhimisha misa ya wafu kwa heshima ya mwanamuziki nyota wa muziki wa Soukus na Rhumba raia wa Jamhuri ya Congo Papa Wemba. Waomboloezaji walipiga foleni ilikupata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa msanii huyo nguli aliyeaga dunia juma lililopita alipokuwa akiwatumbuiza mashabiki wake huko Abidjan Ivory Coast. Mwili wake umewekwa katika majengo ya bunge mjini Kinshasa. Serikali imetangaza siku tatu za maombolezi kuanzia leo hadi jumatano atakapozikwa. Tayari amepewa tuzo kwa mchango wake. Maelfu watarajiwa kujitokeza kumuaga Papa Wemba Faly Ipupa na mashabiki waulaki mwili wa Papa Wemba Historia ya Papa Wemba Msanii huyo nguli alikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa Soukus nchini DRC na kote duniani kwa kipaji chake cha kipekee na sauti isiyokuwa na mfano. Wengi waliitambua sauti hiyo ya na utunzi wake. Alikuwa ni mtumbuizaji kamili.  Gwiji huyo wa muziki wa Lingala aliz

MKUU WA CHUO CHA UHASIBU AFUNGWA KWA KOSA LA KUAJIRI WATUMISHI WENYE ELIMU YA DARASA LA 7

Image
MKUU wa Chuo cha Uhasibu (IAA) Njiro mkoani Arusha, Profesa Johannes Monyo amehukumiwa kifungo cha nje kwa sharti la kutofanya kosa lolote ndani ya mwaka mmoja. Hukumu hiyo ilitolewa Ijumaa iliyopita na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Devotha Msofe baada ya kujiridhisha kuwa Profesa Monyo alifanya makosa ya kuajiri watumishi wanane wenye elimu ya darasa la saba bila kufuata misingi na kanuni za utumishi wa umma. Hakimu Msofe alisema Profesa Monyo akiwa Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Njiro, aliwaingiza watumishi wanane kwenye ajira ya kudumu bila ya kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi au Katibu Mkuu Utumishi. Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani kwa mashahidi 10 pamoja na vielelezo vinane vilivyotolewa mahakamani hapo na upande wa mshtakiwa kuwa na mashahidi wawili, mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka kuwa Profesa Monyo alifanya kosa hilo la kuajiri wafanyakazi hao wanane bila kufuata taratibu za kisheria. “Mahakama imejiridhisha pasip

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANITAREHE 3/5/2016

Image