Posts

Showing posts from July 23, 2018

BREAKING: SANGA ATANGAZA RASMI KUACHIA NGAZI YANGA

Image
Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa wake katika klabu hiyo. Sanga amejiuzulu wadhifa huo kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri baina yake na viongozi wenzake ndani ya klabu hiyo ikiwemo wale wa Kamati ya Utendaji kueleza hana ushirikiano mzuri. Kiongozi huyo aliyekuwa akikaimu nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, alikuwa akitupiwa lawama na viongozi wa Kamati ya Utendaji akiwemo Khalfan Hamis ambaye amejiuzulu juzi akidai Sanga amekuwa si mweledi wa mambo. Mbali na kukosa maelewano, Sanga ameeleza kuwa kuna CLIP ameiona mitandaoni inayohamasisha watu kumvamia kwa mapanga ni moja ya sababu zilizopelekea kufanya uamuzi wa kuachia ngazi. Aidha,wiki kadhaa zilizopita Mjumbe mwingine kutoka kamati hiyo, Salum Mkemi naye aling’atuka kuendelea na wadhifa huo ndani ya Yanga na akisalia kuwa mwanachama pekee kutokana na kutokuwa na kukosa maelewano mazuri baina yake na wanachama wa klabu. Ukiachana na Sanga, Kati...

Rais Magufulia atoa agizo kwa Mkandarasi Daraja la Salender

Image
Rais John Magufuli amemuagiza Mkandarasi aliyepewa kazi wa kujenga daraja kubwa la Selander Bridge kutoka Coco Beach mpaka Agha Khan litakalogharimu shilingi bilioni 250 kwa ufadhili wa Serikali ya Korea kusini kukamilisha kazi hiyo kwa wakati ndani ya miezi 36 aliyopangiwa  kufanya kazi. Rais Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kushuhudia mkataba wa utiaji saini ujenzi wa darala hilo ambalo litakuwa na urefu wa kilomita 6.23 mbele ya Waziri Mkuu wa Korea Kusini Mh.0 Lee Nak-Y eon Ikulu jijini Dar es Salaam na kusema kukamilika kwa daraja hilo kutaendelea kubadilisha taswira mpya ya Jiji la Dar es Salaam katika miundombinu ya barabara. Katika tukio jingine, hivi sasa Rais Magufuli anapokea gawio la kipindi cha mwaka 2017/18 kutoka Wakala, Kampuni, Taasisi na Mashirika ya Umma 47 ambayo Serikali inamiliki hisa.

Tanga: Diwani wa CUF Avuliwa Udiwani kwa Kutofika Vikaoni

Image
HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imemuondoa kwenye nafasi yake, Diwani wa Kata ya Ngamiani Kusini, Mussa Mbarouk,  ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, baada ya kupoteza sifa kwa kutohudhuria vikao sita mfululizo. Kata hiyo sasa imetangazwa kuwa wazi. You May Like

Madiwani wapita bila kupingwa Uchaguzi mdogo wa Udiwani- Mbulu.

Image
  Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbulu ndugu Hudson S. Kamoga akisoma taarifa ya maamuzi ya rufaa za Wagombea Udiwani katika kata za Tumati na Hayderer . Akiongea na vyombo vya habari hii leo ofisini kwake Msimamizi wa Uchaguzi   jimbo la Mbulu, ndugu Hudson Stanley Kamoga amewatangaza Madiwani wawili wa kata ya Tumati ndugu Paulo Emanuel Axwesso (CCM) na ndugu Justine Sidamuy Masuja Hayderer(CCM),wamepita bila kupingwa   baada ya Wapinzani wao kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushindwa rufaa waliokata Tume ya Taifa ya Uchaguzi dhidi ya Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi.   Msimamizi msaidi wa jimbo la Mbulu ndugu Michael Faraay(wa kwanza kushoto) akiwa na mratibu wa uchaguzi ndugu Stedvant Kileo wakimsikiliza kwa makini msimamizi wa uchaguzi (hayupo pichani)wakati wakusoma maamuzi ya rufaa Akitoa taarifa juu ya maamuzi ya rufaa hiyo iliyotolewa na tume ya taifa ya Uchaguzi,msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ame...