KIFO CHA TYSON CHAMLIZA ZAIDI MBONI, AY AOKOA JAHAZI
Mtangazaji wa kipindi cha Mboni Show, Mboni Masimba akilia kwa uchungu akiwa nje ya Hospitali ya Mkoa wa Morogoro wakati wakisubiri kusafirisha maiti kuelekea Dar. Marehemu Tyson ndiye alikuwa Mtayarishaji wa kipindi chake na walikuwa wote katika safari hiyo, ingawa walikuwa magari tofauti. Mboni (kushoto) akiwa na Mtangazaji wa ITV, Devota Minja Mboni akifarijiwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka. AY AOKOA JAHAZI Katika hatua nyingine, msanii wa Hip Hop nchini, Ambwene Yessaya 'AY' (anayehesabu pesa) aliamua kujitole kununua jeneza la kusafirishia mwili w marehemu, jeneza hilo liligharimu kiasi cha shilingi laki sita ambazo AY alizitoa cash! .....wakisaidiana kubeba jeneza hilo kuelekea hospitalini baada ya kulinunua Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba (mbele), akiongozana na AY kuelekea hospitalini (PICHA: Dastun Shekidele/GPL Morogoro)