BREAKING NEWS: PROF. KITILO AKATAA KUGOMBEA URAISI ACT, BARUA YAKE HII HAPA
Ndugu Wazalendo, Naomba niwashukuru nyote kwa imani kubwa mliyo nayo juu yangu katika kukiwakilisha chama katika nafasi ya Rais. Naishukuru pia Kamati Kuu kwa imani yake kwangu hata kufikia hatua ya kupitisha azimio la kuniomba nigombee urais kwa chama chetu. Jana Kamati Kuu ilituma ujumbe maalumu nyumbani kwangu kwa ajili ya kuzungumza na familia na jamaa zangu juu ya ombi hili. Aidha, Nimekuwa nikilitafakari jambo hili tangu Alhamisi nilipoombwa rasmi kutafakari uwezekano wa mimi kugombea baada ya juhudi zetu za kutafuta mgombea kushindikana. Nimefanya mawasiliano mapana katika familia, ndani ya chama, chuoni ninapofanyia kazi, Kanisani kwangu,na kwa watu na taasisi mbalimbali ninazohusiana nazo. Baada ya tafakari na mawasiliano CONSULTATIONS mapana nasikitika kusema kwamba sina utayari na maandalizi ya maana ya kisaikolojia, kifamilia, na kisiasa kuniwezesha kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi huu. Najua nimewaangusha sana katika uamuzi ...