Kesi ya Madawa: Shahidi Afunguka Alichokikuta Chumbani kwa Wema
Msanii wa filamu, Wema Sepetu (katikati) akiwa na mama yake mzazi Miriam Sepetu (kulia) wakitoka kusikiliza kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mama mzazi wa Wema Sepetu akishuka ngazi za mahakama baada ya kusikiliza kesi inayomkabili mwanaye. Wema Sepetu na mama yake, Miriam Sepetu wakijadili jambo baada ya kusikiliza kesi nje ya mahakama. MJUMBE wa Shina Namba 39, nyumbani anakoishi msanii wa filamu, Wema Sepetu, Steven Alphonce ambaye ni shahidi katika kesi inayomkabili staa huyo, amedai wakati wa upekuzi walikuta kipande cha sigara wala si bangi. Alphonce amesema hayo leo Jumatatu, Machi 12, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, wakati akitoa ushahidi wake katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Wema na wenzake wawili na kusema alishiriki katika upekuzi nyumbani kwa Wema na kukuta kipande hicho cha sigara jikoni n...