Posts

Showing posts from February 23, 2018

Kauli ya Zitto Kabwe baada ya kuachiwa

Image
Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka na kuwataka watu wasirudishwe nyuma kwa vitisho na usumbufu wa sheria kandamizi zinazopelekea baadhi ya viongozi kukamatwa na kuwekwa ndani. Zitto Kabwe ameweka wazi hayo mara baada ya kuachiwa leo Februari 23, 2018 na kusema kuwa yeye anaendelea na harakati zake ya kuwafikia viongozi na Kata ambazo wananchi waliwachagua viongozi wa ACT Wazalendo. "Tusirudishwe nyuma na vitisho, usumbufu na sheria kandamizi. Harakati za kulinda Demokrasia yetu na Uhuru wa kukusanyika, kujieleza na kupashana habari lazima ziendelee. Ni wajibu wetu kulinda Demokrasia ya Vyama vingi na kuiimarisha iwe madhubuti kwa ajili ya Maendeleo ya Watu wetu. Baada ya kulala bure jana polisi Morogoro, tunaendelea na kazi yetu ya kutembelea kata zote ambazo Wananchi walitupa dhamana kwa kuchagua madiwani wa Act Wazalendo" alisema Zitto Kabwe Aidha Zitto Kabwe ameonyesha kuguswa na muaji mengine ambayo yametokea jana ambap

Vigogo waliokamatwa kwa amri ya RC Mnyeti wahamishiwa Babati

Image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Agustino Senga   Vigogo watano wa madini ya Tanzanite wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro na jijini Arusha, walioshikiliwa na Polisi kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, wakidaiwa kudhamini uchimbaji haramu wa madini hayo, wamepelekwa mjini Babati chini ya ulinzi wa polisi. Wiki mbili zilizopita Mnyeti aliagiza vigogo hao wa madini kukamatwa na kushikiliwa kwa saa 48 kwenye kituo cha polisi Mirerani wakidaiwa kufadhili uchimbaji huo haramu. Akizungumza leo Februari 23, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Agustino Senga amethibitisha vigogo hao wa madini kusafirishwa licha ya kuwa walipatiwa dhamana, polisi wakawashikilia na kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo. Amesema waliwashikilia wachimbaji hao baada ya kamati iliyoundwa na mkuu wa mkoa huo kupata taarifa kuwa vigogo hao wanashiriki kuwadhamini vijana wanaoingia kwa wizi kwenye migodi ya kampuni ya TanzaniteOne yenye ubia na Ser

BREAKING : POLISI AUAWA KWENYE VURUGU ZAMASHABIKI

Image
Afisa Polisi mmoja amefariki hapo jana kufuatia vurugu zilizofanywa na baadhi ya mashabiki wa klabu ya Spartak Moscow dhid ya wale wa timu ya Athletic Bilbao kabla ya mchezo wa Europa League hapo jana siku ya Alhamisi. Watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kuwasha baruti zilizokuwa zikiwaka katika mitaa zilizosababisha baadhi ya mashabiki wa Bilbao kufikishwa hospitali. Kufuatia machafuko hayo askari polisi mmoja alifariki kutokana na shinikizo la moyo. Msemaji wa jeshi la polisi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho huku akishindwa kueleza chanzo cha umauti wake. Askari huyo alifariki baada ya kufikishwa hospitalini kwaajili ya matibabu8 kufuatia kupata shinikizo la moyo wakati akijaribu kutuliza vurugu za mashabiki eneo la Basque. Shirikisho la soka barani Ulay (UEFA) limesema kuwa limesikitishwa na tukio hilo lililojitokeza huko Bilbao usiku wa siku ya Alhamisi.

Zitto Aachiwa kwa Dhamana, Atoa Kauli Mauaji ya Diwani

Image
KIONGOZI Mkuu wa  ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameachiwa kwa dhamana ya maneno ya Sh. 50 milioni na kudhaminiwa na wakili wake, Lazarus Mvula baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi Morogoro tangu jana Alhamisi kwa kufanya mkusanyiko bila kibali. Zitto alikamatwa katika Kata ya Kikeo wilayani Mvomero na alitarajiwa kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dakawa lakini akahamishiwa Morogoro Mjini. “Muda huu ameachiwa kwa dhamana ya maneno yenye thamani ya Sh50milioni. Anatakiwa kuripoti Polisi Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro Jumatatu, Machi 12, 2018,” inaeleza taarifa ya wakili wake. Aidha, Zitto amefungukia mauaji ya Diwani wa Kata ya Namawala wilayani Kilombero, Godfrey Luena (CHADEMA) ameuawa usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.

Mwandishi wa Gazeti la Uhuru ajeruhiwa Ajali ya Malori

Image
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru, Mariam Mziwanda, amejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu, eneo la Tabata TOT jijini Dar es Salaam, usiku huu baada ya gari dogo alilokuwa akiliendesha lenye namba za usajili T222 DJX kugongana na lori la mizigo lenye namba za usajili T 495 na kisha kuingia katikati na kubanwa na lori la mafuta lenye namba za usajili T 748 BMT. Kwa mujibu wa dereva wa lori la mafuta lililohusika katika ajali, William Colonel, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa lori la mzigo ambalo liliacha njia na kupanda kingo za katikati ya barabara, kisha kupinduka na kuangukia lori la mafuta na gari lililokuwa likiendeshwa na Mziwanda. Lori la mafuta na gari dogo yote yalikuwa upande wa kushoto wa barabara. Imeelezwa lori hilo baada ya kuanguka lililibana gari dogo lililokuwa katikati. Shuhuda wa ajali hiyo, Adeodatus Sylivester Charles amesema "Nilimtambua majeru

JPM: Mtanisamehe, Mimi Siyo Mwanasiasa Mzuri!

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa yeye si mwanasiasa mzuri ndiyo maana lugha yake siku zote si nzuri. Magufuli amesema hayo leo Februari 22, 2018 wakati akihotubia katika mkutano wa 19 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao unaendelea sasa Kampala nchini Uganda ambapo Marais wa nchi hizo wamekutana huko kujadili mambo mbalimbali ambapo Rais Magufuli amewataka viongozi hao kuangalia changamoto mbalimbali ambazo zinazikabili nchi hizo. “Mtanisamehe lugha yangu siyo nzuri kwa kuwa mimi siyo mwanasiasa mzuri, tunataka kutengeneza viwanda yaani kuzifanya nchi zetu ziwe za viwanda tutaweza kushindana na nchi ambazo gharama yake ni 0.12 wakati sisi ni zaidi ya mara kumi ya hiyo hayo ni maswali ambayo sisi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kila mmoja wetu lazima tujiulize je tutafika hapo hizo ndiyo changamoto lakini pia gharama za umeme zinasababisha gharama za uzalishaji kuongezeka na kupelekea pato l

Rais wa FIFA atoa ahadi hii kwa Majaliwa

Image
Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino amemwahidi Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kuwa FIFA itawekeza katika miradi ya maendeleo ya soka nchini. Infantino ametoa ahadi hiyo jana katika mazungumzo yake maalum na Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa ofisini kwake baada ya kumtembelea ikiwa ni sehemu ya ratiba zake nchini baada ya kumaliza mkutano mkuu wa FIFA wa mwaka wa kikanda. Kwa upande wake Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania inaunga mkono juhudi za FIFA katika kupambana na rushwa kwenye soka pamoja na matumizi mabaya ya fedha na madaraka. Rais huyo aliyechukua mikoba ya Mswisi Joseph ‘Sepp’ Blatter Februari 26 mwaka 2016 ameunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania kupambana na rushwa katika sekta ya michezo. Aidha Infantino ameishukuru Serikali kwa ukarimu wake na kumuomba Waziri Mkuu Majaaliwa kufikisha salamu za shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe

Breaking News: Diwani Chadema Auawa Usiku Morogoro

Image
Diwani wa Kata ya Namawala wilayani Kilombero, Godfrey Luena (CHADEMA) ameuawa usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana. Kwa mujibu wa mbunge wa Kilobero, Peter Lijualikali amesema; Taarifa za awali zinasema kuwa usiku huu umeme ulikatika katika nyumba yake. Luena akatoka nje kutizama kama kuna shot maana nyumba za jirani zilikuwa na umeme. Alipozunguka nyuma ya nyumba yake kukagua umeme akalutana na kikosi cha watu wenye mapanga wakamkatakata hadi wakamtoa roho. Ameandika Mbunge wa Mikumi @professorjaytz ameandika; “Diwani wetu wa Chadema Kata ya Namwawala, Jimbo la MLIMBA (MOROGORO) GODFREY LUENA ameuawa usiku huu nyumbani kwake kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana,   R.I.P. LUENA.” Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limethibitisha kutokea kwa kifo hicho; “Ni kweli diwani Luena ameuawa usiku wa huu, polisi wameshafika eneo la tukio wanaendelea na uchunguzi lakini ni mapema sana kutoa majibu kwamb