EXCLUSIVE: JOHARI AJIFUNGUA KWA SIRI
Mshtuko! Baada ya kujulikana kwa wengi kuwa hana mtoto na madai ya kutokuwa na uwezo wa kuzaa, mwigizaji wa kitambo Bongo, Blandina William Chagula ‘Johari’ ameshangaza baada ya siri kuvuja kuwa amejifungua kwa siri ambapo mtoto ana umri wa miezi 7 sasa, jambo lililozua mkanganyiko na mjadala mzito, Risasi Jumamosi linakupa ‘exclusive story’. Mwigizaji wa kitambo Bongo, Blandina William Chagula ‘Johari’ UBUYU WAMWAGWA Mwandishi wetu akiwa katika majukumu yake ya kila siku, ghafla alipigiwa simu na chanzo chake cha kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa Johari na kuanika kila kitu huku kikiomba hifadhi ya jina. Mtoto wa Johari. Sosi: Wewe (kikitaja jina la mwandishi) una habari? Mwandishi: Zimejaa tele lakini hiyo yako inaweza kuwa ya muhimu zaidi. Sosi: Tena ni muhimu kweli, unajua kuwa Johari ana mtoto na sasa anatimiza miezi saba? Mwandishi: Unasema? Kajifungua lini na wapi? Sosi: Kitambo tu, mbona hata kwenye ukurasa wake wa Instagram kaweka hizo picha, ...