Posts

Showing posts from July 27, 2017

Ruby Amuanika Baba Kijacho Wake

Image
BAADA ya kufanya vizuri na baadhi ya ngoma zake kama Na Yule , Sijutii, na nyingine nyingi, staa wa Bongo Fleva , Ruby , amemuanika baba kijacho wake kwenye ukurasa wake wa Instagram. . Huyu ndiye Jamali mpenzi wa Ruby Ruby ambaye ‘amejaza na akajazwa’ na sasa ni mama kijacho amemtundika ‘ handsome boy ’ wake huyo anayeitwa Jamal na kumuandikia ujumbe ufuatao. “ My prince charm, my smile maker, Baba princess Ruby ” NA ISRI MOHAMED/GPL

MANCHESTER UNITED WATANDIKWA NA FC BARCELONA,NEYMAR ATUPIA

Image
Neymar celebrates after his first-half goal gave Barcelona the lead against Manchester United at the FedExField Neymar capitalises on a poor first touch Antonio Valencia to bare down on the Manchester United goal United's Ecuadorian right back looks on despairingly as Neymar takes the ball away from him to score the opener Neymar passes the ball home into the United net after getting it out of his feet with Messi watching on  Manchester United's players look dejected in the background as Brazilian superstar Neymar wheels away to celebrate Barcelona starting XI (4-3-3): Cillessen; Semedo, Umtiti, Mascherano, Alba; Busquets, Rakitic, Alena; Messi, Suarez, Neymar. Goal: Neymar 32. Man United (4-2-3-1): De Gea (Romero 46); Valencia (Tuanzebe 88), Lindelof (Jones 46), Smalling (Bailly 46), Blind (Darmian 46); Carrick (Fellaini 46), Pogba; Rashford, Mkhitaryan (Pereira 62), Lingard (Martial 62); Lukaku Booked: Fellaini. Att: 80,162. Lindelof...

Wanawake Watano Wauawa kwa Kuchomwa Moto

Image
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. WANAWAKE watano wameuawa kwa kuchomwa moto Kijiji cha Undomo, Uchama, Nzega mkoani Tabora kwa tuhuma za kuhusika na imani za kishirikina. Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri ameziagiza kamati za ulinzi za mkoa na wilaya kusitisha mara moja kazi zote za sungusungu kwa madai kwamba sungusungu hao wanahusika na mauaji hayo na kuvitaka vyombo vya usalama kuhakikisha vinawakamata na kuwafikisha mbele ya sheria watu wote wanaohusika. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwataja waliouawa kuwa ni Ester Kaswahili, Njungu Maswari, Christina Said, Kabula Kagito. Kamanda Mutafungwa ameeleza kwamba wamewakamata viongozi wa eneo tukio hilo lilipotokea, akiwemo diwani, Ofisa mtendaji wa kata na Ofisa mtendaji wa kijiji kwa madai kwamba walikuwa wakifahamu kinachoendelea kwenye eneo lao lakini kwa makusudi, waliamua kutotoa taarifa kwa jeshi la polisi, j...

BREAKING NEWS: Tundu Lissu Aachiwa kwa Dhamana

Image
  Tundu Lissu akiwasalimia wananchi waliofika mahakamani hapo. MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia kwa dhamana Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) na Rais wa Chama cha Wanasheria nchini, Tundu Lissu mapema leo asubuhi. Lissu ametakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja ataweka bondi ya dhamana ya shilingi milioni 10 huku akiwekewa zuio la kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila kibali maalum cha mahakama. Aidha kesi yake imepangwa kusikilizwa Agosti 24 mwaka huu baada ya wadhamini wake kukamilisha taratibu zote za kumdhamini. Tundu  Lissu ambaye alikamatwa Alhamisi, Julai 20 mwaka huu, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati akijiandaa kuelekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Chama cha Wanasheria cha Afrika Mashariki (EALS), alifikishwa Mahakamani hapo Jumatatu Julai 24 na kusomewa mashtaka  ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Serikali, kosa ambalo anadaiwa kulitenda Julai 17. Inadaiwa kuwa maneno h...