Posts

Showing posts from December 7, 2015

MUHUMBILI YAPATIWA MSAADA WA MASHINE YA KISASA YA DIGITAL YA X-RAY

Image
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu matumizi ya mashine mpya ya X-ray ya digitali.  Dk Lwakatare amesema mashine hiyo ina uwezo wa kupiga picha na kutumwa nje ya nchi kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu zaidi. Mashine hiyo haihitaji chumba cha kusafishia picha wala dawa za kusafishia. Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akitoa maelezo kuhusu idadi ya wagonjwa waliopata huduma ya kipimo cha CT Scan baada ya mashine hiyo kukamilika. Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). ……………………………………………………………………………… Hospitali ya Taifa  Muhimbili (MNH) imepata mashine mpya na ya kisasa ya Digital X-ray ambayo wataalamu wake hawatalazimika kutu

NEC YATAOA TAMKO KUHUSU UCHAGUZI WA WABUNGE ARUSHA MJINI NA HANDENI

Image
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa kufanyika Tarehe 13/12/2015 katika jimbo Handeni na Arusha Mjini, (kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Bw.Clarence Nanyaro kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva(ambaye hayupo katika picha) leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waaandishi wa habari kuhusu taratibu zitakazo tumika katika uchaguzi wa wabunge katika jimbo la Arusha na Handeni.

MAGUFULI ATAJWA HUKO SWEDEN KUWACHONGANISHA MARAIS WENZAKE NA WAPIGA KURA WAO

Image
Dagens Nyheter ni gazeti kubwa kushinda yote nchini Sweden, ndio 'Daily News' lao kwa maana ya jina la gazeti. Katika toleo lake la Ijumaa Desemba 4, habari za John Magufuli zimepamba pia gazeti hilo. Amemwagiwa sifa, na ikaandikwa pia, kuwa Magufuli amewaweka katika wakati mgumu marais wenzake wa nchi jirani kwa vile wapiga kura wao wameonyesha wivu wao kwa Watanzania kupata Rais wa aina ya Magufuli. Hata hivyo, kwenye gazeti hilo, imeandikwa pia, kuwa hata kabla ya kuingia milango ya Ikulu, Magufuli tayari ameshajipatia maadui wakiwamo wa ndani ya chama chake kwa hatua zake anazozichukua, hususan za kubana matumizi ya Serikali.  Habari nzima  unaweza kuitazama kupitia Website ya Hilo gazeti kwa kubofya link hii hapa .Imeandikwa kwa lugha yao. link: http://www.dn.se/nyheter/varlden/president-skaffar-fiender-nar-han-later-kvasten-ga/ Tafsiri ya maelezo waliyoandika  kwa Kiingereza ni kama inavyosomeka hapa chini...... The newly elected Presiden

SAKATA LA MANJI NA COCO BEACH, TAMKO KALI LATOLEWA,WAFUNGUKA MAZITO,HATUA KALI KUCHUKULIWA

Image
JUKWAA HURU LA WAZALENDO TANZANIA (JUHWATA) TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Ndugu waandishi wa habari, Jukwaa limewaalika hapa katika muendelezo wake wa kuunga mkono juhudi za Mh. Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mh. -Dr. John Magufuli. Hivi karibuni mh. Rais ameongoza mapambano makubwa ya kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi na kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika kuliingizia taifa hasara ya mabilioni ya shilingi yaliyopotea. Tunaunga mkono juhudi hizi za Rais wetu na tunamuhakikishia kuwa Jukwaa linamuunga mkono na kwamba tunaomba azidishe kasi zaidi ili wale wote waliokwepa kodi wakamatwe, walipe na kufikishwa katika vyombo vya sheria bila huruma yoyote. Ndugu waandishi wa habari, leo tumewaita hapa dhumuni kuu likiwa ni kuzungumzia uporaji wa maeneo ya wazi yanayotumiwa na wananchi hasa wanyonge. Uporaji huu unafanywa na baadhi ya wafanyabiashara wenye tamaa ambao hutumia nguvu zao za kiuchumi kuwarubuni na wakati mwingine kuwahonga viongozi wetu wachache seri

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA KATIBU MKUU WIZARA YA UCHUKUZI, AVUNJA BODI YA MAMLAKA YA BANDARI (TPA) LEO

Image
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha kwa waandishi wa habari, ripoti Bandari ya Dar es salaam iliyobaini mianya ya ukwepaji kodi ikiwemo ya Makontena 2,387 yaliyopitishwa kati ya Machi na Septemba mwaka jana. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, Ofisini kwake jijini Dar es salaam leo. RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amevunja bodi ya Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) pamoja na kutengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari Profesa Joseph Msambichaka pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Awadh Massawe. Kuvunjwa kwa bodi hiyo kunatokana na utendaji mbovu wa Mamlaka hiyo kwa muda mrefu na kitendo cha kutokuchukua hatua katika vyanzo husika. Akizungumza  na waandishi wa Habari  Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam leo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kutenguliwa kwa ut

KATIBU MKUU TAMISEMI AKAGUA MIUNDOMBINU YA MFUMO WA MABASI YAENDAYO HARAKA

Image
  Katibu Mkuu Ofisini ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akimweleza jambo Mwenyekiti wa Kampuni ya UDA-RT, Bw. Robert Kisena wakati alipofanya ziara kwenye miundombinu ya mfumo wa Mabasi yaendayo haraka kabla kipindi cha mpito hakijaanza mwezi ujao mwisho mwa wiki. UDA-RT ndiyo kampuni itayotoa huduma ya usafiri katika kipindi hicho na tayari imeshanunua mabasi 140. Katibu Mkuu Ofisini ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akikagua miundombinu ya mfumo wa mabasi yaendeyo haraka na kuli ni Mwenyekiti wa Kampuni ya UDA-RT, Bw. Robert Kisena wakati alipofanya ziara kwenye miundombinu ya mfumo wa Mabasi yaendayo haraka kabla kipindi cha mpito hakijaanza mwezi ujao mwishoni mwa wiki. UDA-RT ndiyo kampuni itayotoa huduma ya usafiri katika kipindi hicho na tayari imeshanunua mabasi