Posts

Showing posts from October 11, 2017

MKUU WA WILAYA YA MBULU,ATATUA MGOGORO WA KIMPAKA KATI YA MBULU NA BABATI.

Image
Mkuu wa wilaya ya Mbulu C helestino S. M ofuga jana tarehe 10/10/2017 ametatua mgogoro wa kimpaka kati ya wilaya ya Mbulu na babati ,ambako kulitokea machafuko usiku wa kuamkia jana na kusababisha kubomolewa kwa nyumba mbili.  Mgogoro huo wa Siku ulishatatuliwa na kamati za ulinzi na usalama za babati na Mbulu mnamo mwezi wa sita. Wakuu wa wilaya babati Raymondi mushi na C helestino S. Mofuga walitatua mgogoro huo baada ya kutuma watalaam kutafsiri mipaka ya wilaya hizo Mbulu.  Hata hivyo mgogoro huo uliibuka tena Jana baada ya wananchi kubomoa nyumba mbili kwa madai zimejengwa katika maeneo ya malisho.  Mkuu huyo  wa wilaya ya mbulu amekemea vikali t a bia za kuharibu Mali za watu wengine na kuwaagiza wote waliobomolewa kuripoti kwa mkuu wa wilaya ya babati kwa kuwa wapo babati kiutawala, ili hatua zichukuliwe dhidi ya wahalifu.  Pia mkuu wa wilaya ameagiza viongozi kusimamia mipaka kikamilifu ili kuepusha machafuk...

BAMIA Husaidia Wagonjwa wa Vidonda vya Tumbo.

Image
Watu wanaosumbuliwa na maradhi kadha wa kadha ya mfumo wa chakula kama vile vidonda vya tumbo na mengine yanayofana na hayo wanaweza kupata ahuweni au kupona kabisa ikiwa watakula bamia. Unafahamu kuwa kwa kula bamia unaweza ukawa umejiondoa katika hatari ya kupata maradhi mbalimbali? Bamia ni chanzo kizuri cha Vitamin A na beta carotene ambavyo ni virutubisho vinavyosaidia kuboresha uwezo wa kuona. Bamia inasaidia kuweka kawaida kiwango cha sukari mwilini na nyuzinyuzi zake zinasaidia kurahisisha ufyonzwaji wa sukari mwilini. Pia hudhibiti pia kiwango cha lehemu mwilini na hasa pale inapokuwa mtu ametumia vyakula vingi vyenye mafuta. Husaidia pia kulainisha choo. Vilevile ni mboga ambayo kwa Waafrika huongeza hamu ya kula na hata kurahisisha kazi ya kumeza. Wataalamu wanaeleza kuwa ina virutubisho vinavyoweza kupambana na bakteria wanaoshambulia utumbo na kusababisha vidonda vya tumbo. Pamoja na haya yote bamia huimarisha mifupa, huongeza kinga dhidi ya magonjwa...

Mtoto wa Mwalimu Mkuu Aanika Alivyomkuta Baba Yake Amejinyonga

Image
MTOTO Frank Benedicto (14) ni mtoto mkubwa wa Mkuu wa Sekondari ya Migukulama, Benedicto Lweikiza (45) aliyejinyonga juzi, amesema alitahamaki kumkuta baba yake akiwa amening’inia darini. Lweikiza alijinyonga hadi kufariki juzi saa tisa alasiri katika mtaa wa Kilabela Kata ya Nyatukala wilayani Sengerema mkoani Mwanza. Mwalimu huyo alikuwa anafundisha Sekondari ya Migukulama iliyopo Kata ya Nyanzenda Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema. Mtoto wa marehemu huyo aliyekuwa akiishi na baba yake kwenye nyumba hiyo, anasoma kidato cha kwanza katika Sekondari ya Sima iliyopo wilayani hapo, alisema baada ya kutoka shuleni alikuta mlango wa nyumba yao upo wazi hivyo akadhani baba yake atakuwa kwa majirani. “Asubuhi niliagana vizuri na baba yangu wakati nikienda shuleni, jioni niliporudi ndipo nikakuta baba amejinyonga juu ya dari na kabla sijagundua kitu chochote nilikuta mlango wa nyumba upo wazi nikadhani yupo kwa majirani nilipoingia chumbani sikuamini nilichokiona...

Majambazi Walivyomtwangwa Risasi Mwenzao Mbele ya Polisi

Image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah. ROBERT Massawe (51) , mkazi wa jijini Dar es Salaam, ambaye polisi wanadai ni mtuhumiwa wa uporaji na mauaji, ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wenzake. Kabla ya kuuawa katika majibizano ya risasi, mtuhumiwa huyo anadaiwa alikamatwa akiwa na SMG yenye risasi 24, simu 19 zilizoporwa maeneo mbalimbali na laini za simu 58. Taarifa iliyotolewa jana Jumanne na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issa h imesema mtuhumiwa aliuawa na wenzake saa tisa usiku wa kuamkia jana wilayani Rombo. Alisema mtuhumiwa pamoja na mkewe walikamatwa jijini Dar es Salaam na baada ya kuhojiwa na polisi inadaiwa alieleza matukio ya ujambazi aliyoshiriki na alikubali kuwaonyesha mahali alipoficha bunduki. Polisi imesema simu tatu kati ya 19 wamegundua ziliporwa Moshi na moja alikuwa akiitumia mkewe ambaye anashikiliwa Dar es Salaam. Kamanda Issah alisema aliwaeleza polisi kuhusu mpango wa kufa...

Chadema Yapata Pigo Lingine

Image
Chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa kimeendelea kujiimarisha kwa kuvuna wanachama watano kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) manispaa ya Iringa wakiwa na mikakati ya kuja kulikomboa jimbo la Iringa mjini ambalo lipo chini ya chama cha CHADEMA. Akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama hao kutoka kata ya kitwiru mwenyekiti wa CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya aliwapongeza wanachama kwa kutambua kazi inayofanywa na chama cha mapinduzi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano DR John Pombe Magufuli. “Mimi nimefurahi sana nyie kurudi nyumbani maana mtakuwa na msaada mkubwa sana katika kukijenga chama hapa manispaa ya Iringa ili tuweze kulikomboa jimbo hili katika uchaguzi ujao na hii ndio mikakati yetu” alisema Rubeya. Rubeya aliwaambia wanachama hao kuwa sasa wapo katika mikono salama ya kisiasa tofauti na walipokuwa kwenye chama cha awali na kuwasihi wasiwe waoga katika kufanya kazi za kukijenga chama cha mapinduzi. “CCM ndio chama tawa...

WEMA SEPETU AMSHUKIA VIKALI SOUD BROWN,AMPA MAKAVU IKISA MAMA YAKE

Image
     There is Limits to everything jamani… Sipendi kabisa wen people involve my Mother kwenye mambo ambayo hata hayamuhusu… Niachie mama angu Soudy… I dont like it wen u bother her like dat only for u to record her alafu uje kumuanika like this… Hivi kwani @soudybrown huna mama wa kumfanyia hivyo unavyofanya… Sasa basi jus like da way huwezi mfanyia mama ako basi usiwafanyie na mama wa wenzako… Have some Respect atleast… Like I said kuna limits katika kila kitu… Hayo mambo yako ya Shilawadu yabaki huku kwetu vijana.. Wazazi tuwaache kama walivyo… Umenikera sana kwakweli… Sijapenda hata kidogo.

TANGAZO: VIWANJA VINAUZWA DODOMA MJINI

Image
Viwanja vinauzwa vipo Dodoma maeneo ya Mnada wa zamani njia ya kwenda Kondoa, SQ.M 1 ni 15,000... Ni kilometa 5 kutoka Jamatini. piga simu hii kwa maelezo zaidi.  0754461753

DIAMOND PLATINUMZ NA RICK ROSS WAKINUKISHA,BABU TALEE ASHUHUDIA LIVE

Image
          Meneja @babutale @richforever na @diamondplatnumz wakielekezana Kitu Flani #location #MiamiUSA ras_vegaHatariii mnyamaaa amekutana na mnyamaaa unyamani  

Mifupa ya Binadamu Yakutwa Kwenye Bwawa Mkoani Shinyanga

Image
KAMANDA wa polisi mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Simon Haule amethibitisha kuokotwa kwa viungo vya mwili wa binadamu katika bwawa la maji la Jomu wakati watu wakitafuta maji huko Tinde mkoani Shinyanga. Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Simon Haule alidai kuwa iku ya Jumatatu  watu walipoona viungo hivyo vya binadamu ilibidi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi na wao walifika na kukuta viungo hivyo. “Fuvu la kichwa limepatikana hapo bwawani, taya ya binadamu, mbavu za binadamu kumi na nne. “Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo jeshi la polisi lilichukua hatua za haraka kufika eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi wa awali tukishirikiana na daktari mtaalam wa viungo vya binadamu  “Katika tukio hilo tulikuta viungo hivyo ikiwa pamoja na mfupa mmoja wa sehemu ya paja, mifupa ya mikono na mifupa ya sehemu ya bega ya binadamu,” alisema Simon Haule. Aidha Kamanda Haule alisema kuwa uchunguzi wa t...

ALI KIBA NA MANGE KIMAMBI MAPYA YAIBUKA

Image
              Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake wa ‘Seduce me’ amefunguka na kusema kuwa Tanzania kila mtu ana haki na uhuru wake hivyo hata yeye anajisikia vizuri kuona watu maarufu wanapenda kazi zake na kudai ana haki ya kupendwa na Mange Kimambi Alikiba amedai kuwa Mange Kimambi ni moja kati ya mashabiki zake na kusema anashukuru sana kuona anapenda kazi zake na kumpa nguvu katika kazi zake hizo kwa kutoa ‘support’. Ni kama shabiki wangu na ‘appreciate’ anapenda muziki wangu kwa sababu mimi namuheshimu kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anani ‘support’ kwenye kazi zangu lakini pia kutokana na uhuru hivyo kila mtu ana haki na vilevile mimi nina haki ya kupendwa na mtu yoyote yule, hivyo nina haki ya kupendwa na Mange Kimambi pia” alisema Alikiba Mbali na hilo Alikiba alisema anajisikia vizuri kuona muziki wake unazidi kufika mbali zaidi duniani na kuendelea kufanya vizuri nyumbani Tanzania na Afrika Ma...