Posts

Showing posts from October 24, 2016

PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO LA KUWASILI MFALME MOHAMED VI WA MOROCCO, NCHINI KWA ZIARA YA SIKU TATU

Image
Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI (aliyetangulia mbele) akishuka katika Ndege mara alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ajili ya ziara rasmi ya siku tatu Jijini Dar es Salaam. Mfalme wa Morocco Mohammed VI akipokea shada la maua alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara rasmi ya siku tatu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Mfalme wa Morocco Mohammed VI mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara rasmi ya ya siku tatu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mfalme wa Morocco Mohammed VI wakisimama kwa nyimbo za Taifa na mizinga 21 mara baada ya Mfalme huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara ya siku tatu ...