PANYA ROAD APEWA KIPIGO KIZITO NA WANANCHI, AZINDUKA AKIWA MOCHWARI
Mtoto Isack Ernest (16) anayetuhumiwa kuwa ni mhalifu, maarufu Panya Road, amezinduka akiwa chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari) katika Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam. Isack ni miongoni mwa vijana watano waliopigwa na wananchi wenye hasira kwa madai ya kuiba mali zao hali iliyosabisha apoteze fahamu na kudhaniwa amefariki dunia. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Gilles Muroto, alisema baada ya polisi kupigiwa simu na raia wema kuwa kuna vijana watatu wamefariki dunia, walikwenda eneo la tukio na kuwakuta wakiwa na hali mbaya. “Mmoja wao anayeitwa Kelvin Nyambocha (14) alifariki dunia baada ya kupigwa na kuchomwa moto na wananchi. “Kabla ya kufariki, Kelvin alifuatana na wenzake kwa lengo la kwenda kuangalia tamasha la kuibua vipaji vya muziki wa singeli lililoandaliwa na Radio Clouds Fm lililofanyika Mbagala Zakhem,” alisema ...