VIDEO
WEMA SEPETU AKIWAPOROMOSHEA MATUSI MAZITO WAFANYAKAZI WAKE WA NDANI
STAA wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa
vimbwanga, Wema Isaac Sepetu amezua bonge la timbwili kwa wafanyakazi
wake wa ndani wa kiume na kike akiwemo mlinzi.
Tukio hilo lililonaswa na vifaa vyetu
vya kisasa vya kunasia matukio ya mnato na video, lilijiri juzikati
nyumbani kwa mwanadada huyo, Kijitonyama, jijini Dar na kusababisha
majirani kufaidi sinema ya bure ya matusi ya nguoni.
Ilikuwa majira ya asubuhi ambapo Miss
Tanzania huyo wa mwaka 2006/07, akiwa ametinga dela, nywele bandia
nyekundu na miwani nyeusi, alikuwa amejiandaa kwa ajili ya mtoko lakini
alipoingia kwenye gari lake aina ya Toyota Lexus Harrier ndipo akagundua
tatizo.
Cha kwanza alichogundua ni kwamba gari hilo lilikuwa limeibiwa power window (mashine ya kushusha na kupandisha kioo) zote.
Cha pili ni kwamba alipopiga āstatiā gari hilo lilikataa kuwaka kutokana na kuchokonolewa kwenye betri.
Baada ya kuona hivyo, Wema aliwaita
wafanyakazi wake wawili, mmoja wa kiume na mlinzi na kuanza kuwawashia
moto kuwa walikuwa wakijua kilichoendelea.
Wema alianza kuwahoji kuwa walilifanya
nini gari hilo, waliponyamaza kumjibu ndipo akapandwa na hasira na
kuanza kutoa mkongāoto kwa kutumia chochote alichokutana nacho mbele
yake.
Huku akimmwagia maji machafu yule mlinzi wa kiume na kumpiga kwa dekio
la plastiki, Wema alikuwa akimwaga mitusi mizito ya nguoni
isiyoandikika kutokana na ukali wake.
āMy friend ninyi ni mabogasi kabisa, nawaambia mtaozea Segerea, mnafanya nini hapa ninyi waā¦(tusi) au mnaā¦(tusi kali).
āNinyi ni ā¦(tusi kubwa likihusisha mama zao), mnakaakaa tu hapa waā¦(tusi tena), mnajua bei ya power window? Mnadhani hili ni Toyota? Kwa taarifa yenu hili ni Lexus ā¦(tusi) zenu,ā alisikika Wema akitumia lugha ya matusi ambayo asilimia kubwa hayaandikiki kwa namna yoyote kutokana na kupitiliza.
āNinyi ni ā¦(tusi kubwa likihusisha mama zao), mnakaakaa tu hapa waā¦(tusi tena), mnajua bei ya power window? Mnadhani hili ni Toyota? Kwa taarifa yenu hili ni Lexus ā¦(tusi) zenu,ā alisikika Wema akitumia lugha ya matusi ambayo asilimia kubwa hayaandikiki kwa namna yoyote kutokana na kupitiliza.
Wema aliendelea kuwakimbiza ndani ya fensi akiwapiga huku sauti ya Martin Kadinda (yule meneja wake) ikisikika, āMwache ataruka ukuta, nenda karipoti polisiā.
Huku akiwa mbogo, Wema alimgeukia mmoja wa mbwa wake aitwaye Fiona na kumuwashia moto huku akimmwagia mitusi:
āNa wewe Fiona unakaa hapo hapo unamuuzia nani sura badala ya kulinda mlinzi, sipendi mambo ya kiā¦ (tusi).
Mkurugenzi huyo wa kampuni ya kufyatua filamu ya Endless Fame Production alikwenda mbali na kuwatuhumu wafanyakazi hao kuwa kuna uwezekano wanatumiwa kumhujumu akiahidi kuwakomesha.
Mkurugenzi huyo wa kampuni ya kufyatua filamu ya Endless Fame Production alikwenda mbali na kuwatuhumu wafanyakazi hao kuwa kuna uwezekano wanatumiwa kumhujumu akiahidi kuwakomesha.
āMnatumwa mnapewa pesa ili mnifanyie hiviā¦gari litaibiwaje power window likiwa ndani na ninyi mkiwepo? Waā¦(tusi) sana ninyi,ā alisikika msanii huyo.
Katika hali ya kushangaza, badala ya
kumuwashia moto mlinzi anayehusika na usalama nyumbani hapo, Wema
āalidiliā na wafanyakazi wa ndani tu huku mlinzi naye akishindwa
kumuamulia na kubaki kumtazama tu namna alivyokuwa akikimbizana na
wafanyakazi hao.
Kwa upande wao majirani walikuwa wakila
chabo na kusikitishwa na mvua ya matusi aliyokuwa akiitoa msanii huyo
ambaye ni kioo cha jamii.
āJamani jamani, hivi hajui tuna watoto wadogo ambao hawastahili kusikia matusi makubwa kama anayomwaga? ā
Ukweli Wema anatusikitisha sana kwa
sababu watoto wanajifunza nini kutoka kwake?ā alihoji mmoja wa majirani
hao aliyeomba hifadhi ya jina ili na yeye asije akawashiwa moto na
msanii huyo.
Comments
Post a Comment