Posts

Showing posts from April 4, 2016

Cheki Matukio Yote ya iHeartradio Music Awards 2016

Image
Taylor Swift akishinda mataji mengi zaidi kuliko wengine kwenye tuzo za iHeart Radio 2016 huko Inglewood, California usikua wa kuamkia leo. Taylor na Justin Timberlake wakipongezana. Taylor akipongezwa na mpenzi wake Calvin Harris kwa kupata tuzo. Justin na Taylor wakifurahia. Selena Gomez naye amenyakuwa tuzo. Selena na Taylor wakikumbatiana. Pongezi kwa Msanii Bora wa Kike wa Mwaka, Taylor Jason Derulo akitumbuiza   Justine Bieber akifanya yake jukwaani.   Selena Gomez alishinda taji la Best Triple Threat   Meghan Trainor akitumbuiza wakati wa ugawaji wa tuzo hizo. Trainor akikamua hit song yake ya No Chris Brown alishinda taji la Msanii wa R&B wa mwaka. Nicky Jam alinyakuwa taji la wimbo wa Kilatini wa Mwaka ambapo wimbo wake wa El Perdón alioimba na Enrique Iglesias ndiyo uliyompaisha. iHeartRadio Music Awards 2016 Winners Song of the Year: Blank Space – Taylor Swift Can’t Feel My Face – The Weeknd...

SAKATA la Mabosi wa NHC na EWURA Kulipwa Mshahara wa Milioni 36 Lachukua Sura Mpya Baada ya Wenyewe Kukana

Image
Mabosi  wa mashirika mawili ya Serikali nchini, wanaodaiwa kulipwa mshahara wa Sh milioni 36, wamekanusha madai hayo, huku wakielezea kushangazwa na taarifa hizo wakati hata nusu ya fedha hizo, hawapati. Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu alisema  halipwi mshahara huo. Akijibu hoja za wajumbe wa kamati hiyo kuhusu taarifa ya utekelezaji na utendaji wa shirika hilo kwa mwaka 2014/15, Mchechu alisema shirika hilo pamoja na kutekeleza majukumu yake, bado lina changamoto za uhaba wa fedha. “Katika ujenzi wa nyumba zetu, Serikali haigharamii masuala ya miundombinu kama vile maji, umeme, barabara hilo ni jukumu letu na linatugharimu fedha nyingi.  “Sasa nashangaa wako watu wanasema mimi nalipwa mshahara mkubwa, sielewi wametoa wapi huo mshahara kwa sababu silipwi mshahara ...

Mange Kimambi Ajitokeza na Kufafanua Kwanini Aliamua Kubadilika na Kuwafanyia Kampeni CCM Wakati wa Uchaguzi Instagram

Image
Mangekimambi_   Waliokuwa wananijua Kabla ya kampeni za Uchaguzi 2015 wanajua nilikuwa nawakosoa CCM daily Tena Kwa Maneno makali mpaka watu walishangaa nilipatwa n a nini kuwafanyia CCM kampeni insta. Kilichonipata first and foremost ni upinzani kubeba uchafu wooote uliokuwa CCM. Ni upinzani kukosa credibility kuliko hata CCM. Nikakaa nikafikiria 2 things who would I rather support Lowassa or Magu. Secondly, I knew for a fact kumsupport Lowassa ni kujichafua bure Na kupoteza muda because he can't win. Yani Hata 90% ya kura zingekuwa zake still asingeshindaaaaaa, just like ZnZ. Yani nilikuwa nawashangaaaaa wale waliokuwa wanajitoa CCM Kwa mbwembwe Thinking they are going to win. Like it's impossible for anyone to win against CCM under current conditions. Hata malaika ashuke leo awe mgombea wa upinzani still CCM watashinda tu. Nilicho realize Ni kwamba watanzania wengi wanajua umuhimu wa katiba kubadilishwa Ila pia hawajui just how much! I think Hata upinzani N...

ZIMWI la Escrow Lazidi Kumwandama Mbunge Anna Tibaijuka Atakiwa Kulipa Kodi ya Shilingi Milioni 586...Mwenyewe Atoa Kauli Hii

Image
Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amesema yupo tayari kulipa kodi ya mapato ya Sh586 milioni iwapo Mahakama itaamuru hivyo. Kodi hiyo inatokana na Sh1.617 bilioni alizopewa  na mfanyabiashara maarufu nchini, James Rugemalira  ambazo zilidaiwa kuchotwa katika akaunti ya Tegeta Escrow. Profesa Tibaijuka aliyasema hayo jana baada ya taarifa kwamba Bodi ya Rufani ya Kodi Tanzania (TRAB), imeagiza utekelezaji wa suala hilo ili kutimiza matakwa ya sheria kuhusu mapato nchini. “Ni kweli ninadaiwa kodi ya Sh586 milioni, ila nimeenda mahakamani kutaka ufafanuzi kama ni halali kufanya hivyo kwa fedha zilizotokana na mchango,” alisema Profesa Tibaijuka na kuongeza “Nilipewa fedha kwa ajili ya shule lakini nadaiwa kama ni kipato binafsi, hivyo nataka Mahakama iseme, ikikubali nitalipa bila shida yoyote.” Mbunge huyo alifafanua kuwa, anatambua kulipa kodi ni suala la kila mwananchi na anachotaka ni ufafanuzi wa uhusiano uliopo kati ya mapato na ...

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 04.04.2016

Image