Posts

Showing posts from November 23, 2013

"BREAKING NEWZ" PROF. BAREGU NAYE PIA AJIUZULU CHADEMA....MAJANGA HAYA CHADEMA!!!!

Image
 Habari zilizotufikia katika chumba chetu cha habari zinaeleza kuwa Mjumbe wa tume ya mabadiliko ya Katiba kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) ametoa kauli ya kujiondoa na kujiuzulu nafasi zake ndani ya Chama hicho kupelekea maamuzi yaliyofanywa na kikao cha kamati kuu ya chama hicho Huyu ni Mjumbe wa pili wa kamati kuu ya Chadema kuamua kujiuzulu wadhifa wake katika kipindi kisichozidi masaa 12. ENDELEA KUWA NASI KWA KULIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK ILI UPATE HABARI ZAIDI

MHE ZITTO KABWE, DK KITILA MKUMBO KUKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI KESHO

Image
Mheshimiwa Zitto Kabwe. Taarifa imetolewa kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe pamoja na Dk Kitila Mkumbo watakutana na wahariri na waandishi wa habari kesho siku ya Jumapili tarehe 24 Novemba 2013. Watatumia nafasi hii kutoa maoni na msimamo wao kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA ya hivi karibuni. Mkutano huu na waandishi wa habari utafanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 5.00 asubuhi. Imetolewa na ofisi ya Mbunge Zitto Kabwe, Dar es Salaam. Jumamosi, 23 Novemba 2013. Dar es…

RAIS WA TFF AMEMPA SIKU 14 RAGE KUITISHA MKUTANO WA DHARURA KUANZIA LEO

Image
Rais wa TFF, Jamali Malinzi. Rais wa TFF, amempa Ismail Rage kuitisha mkutano mkuu wa dharura ndani ya siku 14 kuanzia leo kujadili mgogoro wa kiungozi unaoendelea klabuni hapo.

BAADA YA KUVULIWA CHEO CHADEMA, DK KITILA ASEMA BADO YUPO IMARA

Image
Dk. Kitila Mkumbo.   Juu ni ujumbe aliouandika Dk. Kitila Mkumbo kupitia akaunti yake ya Facebook baada ya kuvuliwa Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chadema jana pamoja na baadhi ya maoni ya wadau kuhusiana na ujumbe huo.

KINANA AFANYA ZIARA KIJIJI CHA LITUHI

Image
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya jinsi ya kutumia vifaa vya maabara katika kufanikisha kutambua kemikali kutoka kwa wanafunzi wa kidato cha nne Erasto Ndumba na Stella Hyera wa shule ya sekondari ya Kata ya Mtakatifu Paul kata ya Liuli wilaya ya Nyasa  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi nyumba za madaktari zilizochini ya mradi wa Taasisi Benjamini Mkapa katika kituo cha afya  Mkili kata Liundi wilayani Nyasa.  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishauri jambo kabla ya kuvuka mtu Ruhuhu kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mwenyekiti wa CCM Ndugu Oddo Mwisho.  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Ndugu Ernest Kahindi wakivuka kwa mtumbwi kuelekea kijiji cha Kipingu wilaya ya Ludewa. (P.T)  Katibu wa NEC Si...

KOPE BANDIA ZAMPOFUA MACHO MREMBO

Image
Khadija Omar, mkazi wa Kigogo amepata pigo kufuatia kupofuka macho. AMA kweli hujafa hujaumbika, mrembo Khadija Omar, mkazi wa Kigogo, Dar amepata pigo kufuatia kupofuka macho alipokuwa akiwekwa nyusi bandia katika saluni moja iliyopo maeneo hayo, Risasi Jumamosi lina mkasa mzima. Tukio hilo lilitokea Novemba 14, 2013 na kuvuta hisia za watu wengi waliosikia na kushuhudia mkasa huo. Akizungumza na paparazi wetu juzi huku akimwaga machozi, Khadija alisema siku ya tukio saa 11 jioni alikwenda kwenye saluni hiyo iliyopo jirani na anapoishi kwa lengo la kubadili mwonekano wake wa macho kama akina dada wengine wanavyofanya. “Mara tu baada ya kunibandika kope nilianza kuona giza, nikawaeleza akina dada waliniweka lakini wakanipuuza na kuniambia mimi ni mwoga. “Muda mfupi mbele hali yangu ikawa mbaya zaidi, ikabidi wazibandue kope lakini juhudi zao ziligonga mwamba kwa sababu...

Mtikisiko Chadema:Baada ya Zitto kuwekwa benchi, Arfi ang'atuka.

Image
Mgogoro ndani ya Chadema umezidi kupamba moto baada ya Kamati Kuu kuwavua uongozi Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo, huku Makamu Mwenyekiti Taifa, Said Arfi akiandika barua ya kujiuzulu. Zitto alivuliwa uongozi wa Naibu Katibu Mkuu Taifa na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wakati Dk Mkumbo amevuliwa ujumbe wa Kamati Kuu. Wawili hao wanatuhumiwa kukisaliti chama. Taarifa zilisema hoja ya kukisaliti chama pia ilimkumba Arfi akidaiwa kumwezesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kupita ubunge bila kupingwa, katika uchaguzi mkuu uliopita na ndiyo sababu ya kuamua kuachia ngazi nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa. Mbali ya kuwavua uongozi Zitto na Dk Mkumbo, pia Kamati Kuu imewapa siku 14 wajieleze kwa nini wasifukuzwe uanachama. Kwa uamuzi huo Zitto amebaki na wadhifa wa ubunge wake wa Kigoma Ka...

DIAMOND: SITUMII KINGA, NASAKA MTOTO!

Image
Stori:  Shakoor Jongo na Musa Mateja HUWEZI kumkwepa Diamond katika ulimwengu wa habari! Staa huyo wa muziki wa Bongo Fleva ambaye jina alilopewa na wazazi wake ni Nasibu Abdul, ameibua mengine mapya, akidai hapendi kabisa kutumia kinga awapo faragha. Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz'. Akizungumza na Risasi Mchanganyiko kwa njia ya simu wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, Diamond katika maelezo yake, alionesha wazi suala la afya yake siyo ishu sana, muhimu kwake ni mtoto. Penniel Mungilwa ‘Penny’. KILIO CHA MTOTO Diamond alisisitiza kwamba kwa sasa kiu yake kubwa ni kupata mtoto na siyo vinginevyo. “Nashukuru maisha yanakwenda vizuri lakini nitakuwa mwenye furaha zaidi kama nitabahatika kupata mtoto. Mwanamke atakayenizalia, atakuwa amekamilisha furaha yangu,” alisema Diamond. Staa huyo wa singo ya Number One inayosumbua kwenye chati mbalimbali za muziki, alisema siku akiitwa baba, atakuwa amefungua uku...

SAMATTA, ULIMWENGU TAYARI WAPO NA MAZEMBE TUNIS KWA FAINALI YA CAF

Image
TP Mazembe tayati imetua mjini Tunis, Tunisia kwa ajili ya Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji Sfaxien kesho ikiwa na washambuliaji wawili wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emanuel Ulimwengu Ulimwengu na Samatta waliicheza Tanzania, Taifa Stars Jumanne mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe ulioisha kwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na baada ya mechi wakaenda kuungana na klabu yao iliyokuwa kambini Ghana. Baada ya wiki moja ya kambi yake Lizzy Sports Complex mjini Accra, Mazembe iliondoka Jumatano asubuhi na kutua jioni Tunis. Baada ya safari ya saa nne (4) na dakika 45 kwenye ndege, waliwasili Uwanja wa ndege wa Carthage mjini Tunis. Baada ya kuwasili, Robert Kidiaba na Cheibane Traore pamoja na kocha Patrice Carteron walijibu maswali ya Waandishi wa Habari wa Tunisia kabla ya timu kwenda kupumzika hotelini kwa dakika 30 kisha kwenda kufanya mazoezi. ...

TUKIO LA MAUAJI ILALA JIJINI DAR CHRISTINA NEWA AFUNGUKA

Image
 Christina Newa akisimulia mkasa mzima wa tukio la mauaji hayo yalitokea Novemba 19 Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam baada ya mpenzi wake Gabriel Munisi kuwashambulia kwa risasi ndugu wa familia moja na kuwaua watu wawili na kisha yeye mwenyewe kujiua. (Picha na Francis Dande) Christina Newa.  Dada wa Christina Newa, Carolyne Newa ambaye alimpoteza mume wake Capt. Francis Shumila katika tukio hilo, akisimulia maisha ya Christina Newa na mpenzi wake, Gabriel Munisi.  Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani Ilala Bungoni.   Mama mzazi wa Christina Newa ambaye alijeruhiwa na risasi begani akisaidiwa na mtoto wake, Carolyne Newa alipokuwa akirudi nyumbani baada ya kuruhusiwa na madaktari kutoka hospitali ya taifa Muhimbili alipokuwa akipata matibabu.  Pole mama....  Waombolezaji msibani.  Christina Newa akizungumza na wa...

Tanesco yaomba kuongeza bei tena, CTI wapinga vikali

Image
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limeomba kuongeza bei ya umeme kwa asilimia 67.87 ikiwa ni kutoka Sh197.8 kwa Unit mpaka Sh332.06. Hayo yamebainishwa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Felchesmi Mramba, alipokuwa akiwasilisha maombi ya shirika hilo mbele ya Wadau wa Umeme na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura). Alisema kwa sasa uzalishaji wa umeme utokanao na nguvu za maji ni asilimia 13, utokanao na gesi ni asilimia 42 na utokanao na mitambo ya mafuta ni asilimia 45. "Kutokana na kuongezeka kwa gharama za kutoa huduma, wastani wa bei iliyopo ya Sh197.8 kwa uniti, hailingani na wastani wa Sh332.06 kwa unit inayotakiwa kukidhi mahitaji ya sasa," alisema Mramba na kuongeza: "Hii ni pungufu kwa kiasi cha Sh134.25 kwa unit...