Posts

Showing posts from April 6, 2017

RAPA NAYA WA MITEGO NA ZITTO KABWE WAANDIKA UJUMBEE HUU BAADA YA ROMA KUKAMATWA

Image
Baada ya Mbunge wa Mikumi na staa Bongo Fleva  Joseph Haule  ‘Prof Jay’ kutoa taarifa kupitia account yake ya Instagram kuhusu kukamatwa kwa staa mwingine wa Hip Hop  Roma Mkatoliki  katika studio za  Tongwe Records  na watu wasiojulikana, taarifa hiyo imeamsha hisia za watu mbalimbali wakiwepo mastaa wa Bongo Fleva na wanasiasa. Leo April 6 2017 kupitia account zao za Instgram na Twitter Rapa  Nay wa Mitego  na Mbunge wa Kigoma Mjini  Zitto Kabwe  wameyaandika haya.. >>>” Kuvamia Ofisi Za watu, heh.! Kumbe nayo ni Kazi.?!  Nina Imani uko salama mwanangu, Kamanda @roma2030 Sina ata chembe ya wasi wasi. #Wapo.”  – Nay wa Mitego. >>>”Uvamizi wa studio ya Tongwe na kumkamata msanii Roma Mkatoliki ni mwendelezo wa uongozi wa kigangstar na lazima kulaani Kwa nguvu zetu zote.”  – Zitto Kabwe.

Nape kuwaeleza ukweli wapiga kura wake jumamosi hii

Image
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ametoa shukrani kwa wote waliomuunga mkono katika kusimamia haki huku akisema kuwa ataenda kuwaeleza wananchi wake ukweli wote. Shukrani kwa wote mlioniunga mkono katika kusimamia haki. Narudi Mtama kuwaeleza wapiga kura wangu UKWELI WOTE. Ni Jmosi hii tar 8/4/17,” ameandika Nape kupitia Twitter. Marchi 23, Rais Magufuli alimuondoa Nape kama Waziri wa Habari,Sanaa na Michezo na nafasi hiyo kuchukuliwa na Dkt Harrison Mwakyembe aliyekuwa waziri wa Katiba na Sheria. 

Breaking News: Aliyekuwa Kiongozi wa Freemasons Tanzania, Sir Andy Chande Afariki Dunia

Image
Aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya Freemason Tanzania na Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji 'Andy' Chande afariki Dunia. Sir Andy amekuwa mwanachama wa Freemasons kwa takribani miongo 6 tangu ajiunge. Alizaliwa Mombasa, Kenya Mei 7 1928 ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene Mjini, Mkoani Tabora (Tanzania). SIR ANDY CHANDE NA FREEMASONS ​ Freemasons wamekuwa wakitajwa kwenye kila aina ya minong’ono. Tumeona matangazo yakialika watu kujiunga nao kama wanataka kupata utajiri na kuwa watu wenye nguvu. Lakini bado Freemason, imebaki kuwa kitendawili miongoni mwa Watanzania wengi. Leo tunakuletea habari kuhusu Mtanzania maarufu aliyefungua kinywa na kueleza namna alivyojiunga na Freemasons, kundi lililo kongwe duniani. Tayari watu mbalimbali watu wenye hamu ya kupata utajiri wamekuwa wakitoa ushuhuda kuhusu kundi hilo na kusikika kwenye vyombo vya habari, hasa baada ya kifo cha mwingizaji nyota, Stephen Kanumba, mwaka 2012. Siyo hiv

MARAIS WALIOUAWA KWA KUPIGWA RISASI WAKIWA MADARAKANI

Image
Tunawaletea marais waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa madarakani. ABRAHAM Lincoln; alikuwa Rais wa 16 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1865 jijini Washington kwa kupigwa risasi kichwani kwa nyuma na John Wilkes. Alikuwa amekaa na mkewe. Bastola iliyotumika inaitwa Deringer.  INDIRA Priyadarshini Gandhi; Alikuwa Rais wa India. Aliuawa mwaka1984 kwa kupigwa risasi na walinzi wake, Satwant Singh na Beant Singh jijini New Delh, India.  JOHN Francis Kennedy ‘JFK’; ni Rais wa 35 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1963 mjini Dallas kwa kupigwa risasi na Lee Harvey akiwa kwenye gari la wazi barabarani. LAURENT Desire Kabila; alimng’oa madarakani Rais Mabotu Seseko wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, lakini mwaka 2001 akauawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa ni walinzi wake.  THOMAS Isdor Noel Sankara; alikuwa Rais wa Burkina Faso Alitawala nchi kwa miaka 4 hadi 1984 alipouawa kwa kupigwa risasi inasemekana alihusika kufanya mauaji hayo ni rafiki yake wa k
Image
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Job Ndugai  ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe (CHADEMA)  Halima Mdee  kujibu tuhuma za kutoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017. Aidha Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge Freeman Mbowe ameagizwa na Spika Ndugai kufika mbele ya Kamati ya Maadili leo akituhumiwa kutukana bunge kufuatia uchaguzi wa EALA. Pia Kamati ya Maadili leo imemuita DC Arumeru, Alexander Manyeti ambapo anatakiwa kutokeza mbele ya kamati hiyo kwa ajili ya kuhojiwa leo.

mwakyembe asema kuwa tukio la kuvamiwa clouds hawezi kulifumbia macho

Image
Dk. Mwakyembe aliyasema hayo wakati wa mahojiano na Nipashe kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana, muda mfupi baada ya Spika wa Bunge kusitisha shughuli za chombo hicho cha kutunga sheria hadi leo saa 3:00 asubuhi. Nipashe ilitaka kujua kinachoendelea kuhusu uchunguzi dhidi ya Makonda ambaye kamati ya watu watano iliyoundwa na aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ilitoa ripoti ikidai Mkuu wa Mkoa huyo alivamia kituo cha TV cha Clouds akiwa na askari wenye bunduki na kutoa vitisho kwa wafanyakazi wa kituo hicho. Kamati hiyo ilidai kubaini Makonda alifanya hivyo ili kulazimisha video ya mwanamke anayedai kuzaa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, irushwe hewani. Katika majibu yake, Dk. Mwakyembe alisema suala hilo ni “zito” na haliwezi kuachwa lipite bila kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua stahiki. Huku akiendelea kuikosoa ripoti ya kamati ya Nape ambayo amekuwa akisisitiza haijakidhi matakwa ya kikatib

Wabunge wapania kumbana Kassim Majaliwa

Image
WABUNGE wa upinzani wamebainisha mambo manane ambayo wamepanga kumbana Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, atakapowasilisha makadirio ya bajeti ya ofisi yake kwa mwaka ujao wa fedha. Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Bunge iliyotolewa Jumatatu na Ofisi ya Katibu wa Bunge, kikao cha leo ambacho ni cha tatu tangu kuanza kwa mkutano wa saba wa Bunge la 11, Waziri Mkuu atawasilisha makadirio ya bajeti yake. Wakizungumza na Nipashe nje ya Ukumbi wa Bunge jana, wabunge wa upinzani walibainisha mambo manane ambayo leo wangependa wapate ufafanuzi kutoka kwa Waziri Mkuu wakati wa mjadala wa bajeti yake. Baadhi ya mambo hayo ni uchunguzi wa miili ya watu iliyoopolewa kwenye Mto Ruvu ikiwa imefungwa ndani ya sandarusi mwishoni mwa mwaka jana, utekelezaji wa kutoa Sh. milioni 50 kila kijiji, kusuasua kwa utekelezaji wa bajeti ya serikali kwa mwaka huu wa fedha, shughuli za serikali kuhamishiwa Dodoma na ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora. KUFYEKWA BAJETI YA B