Meli Yenye Malori 600 ya Kiwanda cha Dangote Yawasili Mtwara
MTWARA: Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dangote Cement Industries ya jijini Mtwara, ambaye pia ni bilionea namba moja Barani Afrika, Alhaji Aliko Dangote jana Desemba 10, 2016 alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Dk Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam alimthibitishia kuwa hana lengo la kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa badala yake anatafuta fursa nyingine za kuwekeza hapa nchini. Katika kuthibitisha hilo, Mfanyabiashara huyo alisema jana kuwa meli yenye malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake mikoani, itawasili nchini. Aliongeza kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini. Baada ya kufanya mazungumzo hayo, meli yenye magari hayo 600 ilitia nanga katika bandari ya Mtwara ambapo ndipo kiwanda cha Saruji cha Dangote kilipo. Aidha, imeelezwa kuwa w...