jeshi nchini Misri limemuondoa madarakani Rais aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia nchini humo Mohamed Morsi na imemteuwa kiongozi wa muda wa nchi baada ya maandamano makubwa yanayoipinga serikali. Akihutubia kwa njia ya televisheni jumatano jioni, mkuu wa jeshi, Abdul Fatah Khalil Al-Sisi alisema katiba ya Misri imesitishwa kwa muda na mkuu wa mahakama ya katiba ameteuliwa kuwa kiongozi wa muda nchini humo. Sisi alitangaza kwamba jeshi linaangalia watu wa Misri kufuatana na maandamano makubwa ya upinzani yakidai kuwa Rais Mohamed Morsi ajiuzulu. Kufuatia hotuba ya kwenye televisheni Bwana Morsi alitoa taarifa kupitia akaunti yake ya Twitter, akiita hatua ya jeshi ni “mapinduzi kamili” . Aliwasihi wa-misri wote kukataa hatua ya jeshi lakini pia aliwataka kuwa na amani. Kiongozi mpya wa muda nchini Misri, Adli Mansour ana umri wa miaka 68 ni mkuu wa sheria katika mahakama ya juu ya katiba. Ataapishwa alhamisi. Kama sehemu...