Posts

Showing posts from February 27, 2017

MBUNGE PAULINA GEKUL APATAA AJALI MBAYA ALAZWA ICU

Image
Mbunge wa jimbo la Babati mjini Paulina Gekul amenusurika kifo baada ya gari lake lenye namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na kupinduka vibaya ambapo mbunge huyo alikuwa katika msafara wa naibu waziri wa Mazingira Luhaga Mpina wilayani Babati mkoa wa Manyara. Baada ya ajali hii kutokea mmbunge Paulina Gekul ambaye ni mmbunge wa babati mjini akakimbizwa hospitali ya mkoa wa manyara na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi I.C.U huku wanahabari wakikatazwa kuingia katika chumba hiki na madakatari ambao wanamuhudumia mbunge huyo Hata hivyo baada ya ajali kutokea naibu waziri wa mazingira amelazimika kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mji wa babati huku mpina akiipongeza halmasahauri ya mji wa babati kwa kutambua umuhimu wa kutunza mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua gari kwaajili ya kubebea taka lenye thamani ya zaidi ya milioni 200.

RAIS YOWERI MUSEVENI AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU MBILI NA KUREJEA NCHINI KWAKE

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kwa ajili ya kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kabla ya kuondoka    ma kurejea nchini kwake.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza kuelekea kwenye ndege mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati nyimbo za Mataifa mawili zilipokuwa zikipigwa katika uwanja w

VIGOGO 4 WA SHIRIKA LA POSTA WATUMBULIWA

Image
BODI ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania, imetengua nafasi tatu za mameneja na ofisa mwandamizi kutokana na vitendo vya umangimeza, urasimu, kufanya kazi kwa mazoea, ubadhirifu na wizi. Mameneja waliotenguliwa ni James Sando ambaye alikuwa Meneja Mkuu, Menejimenti ya Rasilimali. Macrice Mbodo ameteuliwa kushika nafasi hiyo. Mwingine aliyetenguliwa ni Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara Janeth Msofe. Aliyekuwa Meneja wa Mkoa Shinyanga, Hassan Mwang'ombe kateuliwa kushika nafasi hiyo. Bodi pia imewasimamisha kazi Meneja Msaidizi wa Barua na Logistic, Jasson Kalile na Ofisa Mwandamizi wa Usafirishaji, Ambrose John. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo, ameyasema hayo wakatia akizungumza na waandishi wa habari kuwajulisha uamuzi uliofanywa na bodi. Dk. Kondo amesema, imebainika na imewaridhisha kuwa baadhi ya watendaji wakuu wa makao makuu ya Posta wamekuwa kikwazo katika dhana ya uwajibikaji, weledi na kujituma katika