Pretty Kind afungiwa miezi sita kwakutoa Wimbo usio na maadili
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amemfungia msanii Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind kujihusisha na sanaa kwa muda wa miezi sita. Akizungumza leo Jumapili Januari 7 jijini Dar es Salaam, Shonza amesema amechukua hatua hiyo kutokana na msanii huyo kutoa wimbo uitwao ‘viduduwasha’ usio na maadili. Msanii huyo pia amekutwa na kosa la kufanya kazi ya sanaa bila kusajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kuweka mtandaoni picha ya nusu utupu kinyume na maadili. ‘’Kumekuwa na wimbi kubwa la wasanii kutoa nyimbo zenye maneno ya matusi na zisizo na maadili, pamoja wanawake kupiga picha wakiwa wamevaa nusu utupu na kuweka picha hizo katika mitandao,” amesema Shonza na kuongeza, “Nataka kuwapa angalizo wasanii wenye tabia hizi kuwa Serikali inawafuatilia kwa karibu na mwaka huu tumeanza na huyu na wengine wanafuata kama msanii Gift Stanford maarufu kama Gigy Money na Jane Rimoy maarufu kama Sanchi.” Shonza amemta...