NDOA YA MISS TANZANIA, MTOTO WA MAKAMBA… USIPIME!
Victoria Martin na Thuwein Makamba. DAR ES SALAAM: Ni historia! Harusi ya Mrembo aliyetinga Top Five ya Miss Tanzania 2007, Victoria Martin na mtoto wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, Thuwein Makamba imeacha gumzo la aina yake kutokana wawili hao kuangusha sherehe baa’kubwa. NI TANGA Wawili hao walifanya tendo hilo jema kwa Mwenyezi Mungu, Ijumaa iliyopita mkoani Tanga ambapo waalikwa waliizungumzia kama ni ndoa ya kihistoria kwani kwa kipindi hiki, haijawahi kufungwa ndoa na watu kunywa, kula hadi kusaza kwa kiasi hicho. CHANZO KINAIFUNGUKIA Chanzo makini ambacho kilianza kushuhudia sherehe za wawili hao kuanzia send off hadi harusi, kilisema matukio hayo yote yalipambwa na kufuru ya vinywaji na vyakula kiasi ambacho kila aliyeingia ukumbini alitoka akiwa nyang’anyang’a. “Yani kwa kipindi hiki cha Magu (Rais Dk John Pombe Magufuli) sherehe kubwa kuandaliwa kwa kiwango hiki ni tukio la aina yake maana watu kwa kweli hawa...