Posts

Showing posts from March 11, 2015

ZITTO KABWE ALIVYOVULIWA UBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI

Image
Mnadhimu Mkuu Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, akitoa tamko la kumvua uanachama Zitto Zuberi Kabwe leo. Waandishi wa habari wakifuatilia tukio hilo. Lissu akitoa ufafanuzi baada ya kuulizwa maswali na wanahabari. Katibu Mkuu wa Chadema Willbroad Slaa (kulia) akifuatilia mkutano huo wa kumvua uanachama Zitto Kabwe.MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zuberi Zitto Kabwe, amevuliwa uanachama wake mchana huu katika ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jijini Dar es Salaam katika hatua iliyotangazwa na mnadhimu mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu, baada ya mbunge huyo kushindwa kesi iliyokuwa amefungua katika Mahakama Kuu ya Tanzania. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi hizo, Lissu alisema Zitto amefutwa uanachama kwa mujibu wa taratibu na sheria ya chama isemayo kwamba endapo mwanachama atapata tatizo lolote binafsi ama la kichama, malalamiko yote yatasuluhishwa ndani ya chama na si mahakamani. “Hivyo, kwa mujibu...

MUME ASIFIA PENZI LA MISS TANZANIA 2010, SALHA ISRAEL

Image
ALIYEKUWA mume wa mwanamitindo maarufu Bongo, Jacqueline Patrick, ambaye kwa sasa yuko jela nchini China, Abdulatif Fundikira amesifu penzi analopata kutoka kwa mkewe ambaye alikuwa Miss Tanzania 2010, Salha Israel. Miss Tanzania 2010, Salha Israel siku ya ndoa yake. Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, kijana huyo maarufu kama Tiff, alisema hajawahi kujua utamu wa ndoa kama sasa kwani mapenzi anayopata toka kwa mkewe ni ya kiwango cha juu. “Siwezi kukuficha, najisikia raha sana na ninaweza kusema naona raha ya ndoa hivi sasa na kamwe siwezi kujuta kumuoa Salha kwa kuwa ni mwanamke ambaye anajua kumjali mume, namshukuru sana Mungu kunipa mke ambaye ni wa maisha yangu,” alisema.

DIAMOND APATA MSHTUKO DENI LA MIL.800, BARUA YA TRA YAIBUA MAMBO, ZARI WEMA WATAJWA

Image
Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amepatwa na mshtuko mkubwa baada ya kuwepo madai ya kudaiwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 800 na serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili. Mwishoni mwa wiki iliyopita, barua inayodaiwa kuandikwa na mamlaka hiyo halali ya serikali, ilisambazwa mitandaoni, ikielezwa kuwa ilikuwa imetumwa kwa meneja wa msanii huyo ambaye kwa sasa ndiye yupo juu, ikimtaka kupeleka nakala za mikataba yote ya muziki aliyoingia kwa ajili ya kufanya shoo, kuanzia mwaka 2010 hadi sasa. Baada ya kuwekwa kwa barua hiyo mitandaoni, watu mbalimbali walitoa maoni yao walionyesha hisia tofauti, baadhi wakipinga kwa madai kuwa wanamuonea huku wengine wakisema siyo Diamond tu, bali wasanii wote wanastahili kulipa kodi kutokana na mapato wanayopata kupitia kazi zao. KODI ZIPOJE KI...