Posts

Showing posts from December 23, 2017

Haji Manara; kitendo cha Klabu yangu kufungwa kwa penanti ni aibu ya mwaka

Image
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amefunguka na kusema kitendo cha klabu yake ya Simba jana kufungwa kwa njia ya penati na kuondolewa kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup ni aibu ya mwaka. Haji Manara alisema hayo jana baada ya waliokuwa mabingwa watetezi wa (Azam Sports Federation Cup) Simba kupigwa na Green Warriors na kuondolewa katika michuano hiyo kwa penati 4-3 "Shame!! Aibu!!!Fedheha!!! Haivumiliki!!!Tumewakera fans wetu zaidi ya twenty millions... nimeumia kuliko siku zote toka nimeanza kazi Simba..Aibu ya mwaka" aliandika Haji Manara

Mwalimu atiwa mbaroni kwa kubaka wanafunzi wake

Image
Mwalimu mbaroni akidaiwa kubaka wanafunzi wake tisa MWALIMU wa Shule ya Msingi Itiryo, Samweli Bisendo (29),  amekamatwa na jeshi la polisi akituhumiwa kubaka wanafunzi tisa wa shule yake iliyopo wilayani Tarime. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe, alisema kuwa mwalimu huyo anadaiwa kutenda unyama huo kwa nyakati tofauti hadi alipobainika. "Jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mwalimu wa shule ya msingi Itiryo, Samweli Mariba Bisendo (29) kwa tuhuma ya kubaka watoto wapatao tisa ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi Itiryo,” alisema Kamanda Mwaibambe na kuongeza kuwa matukio hayo yalifanyika kati ya Novemba 30 na Desemba 6,mwaka huu. “Alikamatwa wakati akiwa anajiandaa kutorokea nchi jirani ya Kenya," alisema Mwaibambe. Aidha, Mwaibambe alipongeza ushirikiano kutoka kwa wananchi ambao ndiyo waliowezesha jitihada za polisi kuzaa matunda  katika  kumkamata mwalimu huy...

Nabii Amnunulia Binti Yake wa Miaka 4 Gari la Mil. 926

Image
Mtoto Israella Bushiri. NABII wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering, Shepherd Bushiri, amemfanyia sapraizi mwanayae wa kike, Israella Bushiri mwenye umri wa miaka 4, baada ya kumnunulia gari aina ya Maserati Levante lenye thamani ya Sh milioni 926, kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa. Gari alilonunuliwa na baba yake. Bushiri alitumia ukurasa wake wa Facebook ku-share picha na kuandika maneno ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya pekee aliyomjalia kumpata binti yake huyo. Gari lenyewe. Nabii huyo ambaye mara nyingi anafanya kazi zake za uinjilishaji nchini Afrika Kusini aliandika: “Ninaona baraka zako Mungu kwa zawadi hii ya pekee uliyonipa katika maisha yangu. Ninasherehekea kuzaliwa kwa Mungu wangu na mwokozi wangu Yesu Kristo, na kuzaliwa kwa binti yangu wa kwanza, Israella Bushiri. “Ninaona ni kama jana tu wakati mtoto huyu alipozaliwa na kumbeba mikononi mwangu, lakini leo naweza kumweka mabegani mwangu na akatulia mwenyewe pasipo kushikiliwa, nit...

Hamisa Mobetto: “Ungejiamini Wako angetulia”

Image
Kutokana na kile ambacho kinaendelea kwenye mitandao ya kijamii kati ya Zari the bosslady  na Hamisa Mobetto ambao wanadaiwa kuwa wanarushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii kutokana na who wawili kuhost party usiku wa December 21,2017 Kampala Uganda na kusemekana kuwa Zari alijaza watu wengi kuliko Hamisa Mobetto. Hamisa Mobetto aonyesha kuendelea kurusha vijembe kwa Zari kupitia mtandao wake wa snapchat ambapo Hamisa ameandika “Tembo gani anang’olewa pembe kila siku” na Zari kumjibu “vikatuni kumi wanakusanya michango ya kusaidia watoto, vinyago kwenye mitandao ya kijamii,walioshindwa na maisha wakajikusanya kumshusha mtu mmoja,lakini mkashindwa#TheGeneral”

SIMBA KAMA MANCHESTER UNITED, WAVULIWA UBINGWA WA KOMBE LA FA

Image
Kikosi cha timu ya Simba SC. Siku mbili baada ya Manchester United ya England kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Ligi dhidi ya Bristol City inayoshiriki Ligi Daraja la Pili, mabingwa wa Kombe la FA nchini Tanzania, Simba nao wamevuliwa ubingwa wa michuano hiyo kwa kufungwa na Green Warious. Simba imevuliwa ubingwa huo usiku huu wa Ijumaa kwenye Uwanja wa Azam Complex ulipo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kwa njia ya penati 4-3. Hatua hiyo ilifika baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida, ndipo mwamuzi Israel Nkono akaamuru zipigwe penati. Kipa wa Green, Shaban Dihile ndiye aliyekuwa shujaa kutokana na kuonekana kuwa imara langoni huku wachezaji wa Simba, Mzamiru Yassin, Mohamed Hussein ‘Zimbwe JR na Jonas Mkude wakikosa penati na kuchangia timu hiyo ya Ligi Daraja la Pili kusonga mbele dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom. Waliopata penati za Simba ni Erasto Nyoni, Shiza Kichuya na John Bocco.

BREAKING NEWS : ASKARI MWINGINE WA JWT ALIYESHAMBULIWA DRC AFARIKI DUNIA

Image
ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) aliyekuwa katika Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) amefariki dunia nchini Uganda wakati akipatiwa matibabu. Askari huyo ni miongoni mwa askari 44 wa Tanzania waliojeruhiwa katika shambulio lililofanywa Desemba 7 mwaka huu na waasi wa The Allied Democratic Forces (ADF) katika kambi ya walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa (MONUSCO), na kusababisha vifo vya wanajeshi 14 wa Tanzania na watano wa DRC. Msemaji wa Katibu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, alitangaza taarifa hiyo ya kusikitisha katika Makao Makuu wa UN, Mjini New York jana Desemba 22, 2017 usiku. Katika taarifa iliyotolewa na MONUSCO leo, imeeleza kwamba mwanajeshi wa 15 wa Tanzania amefariki dunia akipatiwa matibabu mjini Kampala. Umoja wa Mataifa umetuma salamu za pole kwa wanajeshi, familia, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na serikali ya Tanzania kutokana ...

Mbaroni kwa Kukutwa na Magamba ya Kakakuona na Nyama ya Simba

Image
JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Ngerezya Chamukaga mkazi wa Kijiji cha Kanyara wilaya ya Sengerema kwa kukutwa na nyara mbalimbali za serikali, yakiwemo magamba 40 ya Kakakuona na vipande vitatu vya nyama ya Simba. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi Ahmed Msangi amesema Chamukaga alikamatwa Desemba 21 mwaka huu majira ya saa 1 usiku akiwa na nyara hizo za serikali. Katika tukio jinine, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mukadam Mukadamu ameongoza oparesheni ya ukaguzi wa mabasi ya abiria yaendayo mikoani na nchi za jirani katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Nyegezi, ambapo mabasi matatu yanayosafirisha abiria kuelekea jijini Dar es Salaam yamezuiliwa baada ya kubaini kuwa hayajakidhi vigezo. Baadhi ya madereva wa mabasi yaliyofanyiwa ukaguzi wa leseni na kuwapima kilevi, wameupongeza utaratibu huo na kuomba uwe endelevu, huku abiria pamoja na wadau wengine wa usafiri wakisema ukaguzi h...