Posts

Showing posts from April 25, 2017

Sakata la Bosi wa UN kufukuzwa latua bungeni

Image
Dodoma. Sakata la kufukuzwa nchini la bosi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Awa Dabo, limetua bungeni. Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga(Chadema) akizungumza bungeni leo,  aliitaka serikali kufafanua sababu za kumfukuza nchini Mkurugenzi Mkazi huyo wa UNDP Tanzania kwa kumpa saa 24. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge aliliambia bunge kuwa serikali ina mamlaka yote katika masuala ya kidiplomasia na hivyo bunge haliwezi kuhoji  sababu za mkurugenzi huyo kufukuzwa.

MREMBO DAYNA NYANGE NA GONJWA LA KUWEWESEKA

Image
Staa wa Bongo Fleva, Mwanaisha Saidi ‘Dayna Nyange’. STAA wa Bongo Fleva, Mwanaisha Saidi ‘ Dayna Nyange ’ amefunguka kuwa siku za hivi karibuni amekumbwa na gonjwa la kuweweseka linalomkosesha raha. Akipiga stori na  Uwazi Showbiz , Dayna alieleza kuwa kuweweseka huko kunatokana na msongo wa mawazo alionao kwani anawaza kazi mpya atakayoitoa baada ya Wimbo wa Komelo kuendelea kufanya vizuri kwani muziki kwa sasa una ushindani mkubwa mno. “Kiukweli ninavyowaza kuhusu ujio mpya mpaka najikuta naweweseka usiku wakati nikiwa nimelala, nikishtuka natuliza mawazo na kujipa moyo kuwa Mungu atanisaidia nitaandaa kazi nzuri ambayo itafika mbali zaidi ya hii niliyotoa sasa,” alisema Dayna.

WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WATINGA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON, DC

Image
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo siku ya Jumatatu April 24, 2017 wametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na kukutana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi. Katika picha toka kushoto ni Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bi. Swahiba Mdeme,Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania na Canada Col. Adolph Mutta, Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa A. Ghasia, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi, Mbunge Mhe. Janeth Z. Mbene, Mhe. Josephat S. Kandege, Afisa wa Ubalozi Bwn. Dismas Assenga na Afisa wa Bunge Bwn. Godfrey Godwin. Wabunge hao wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania walikuja Washington, DC kuhudhuria mikutano ya kipupwe ya Benki ya Dunia na IMF Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi. Katika picha toka kushoto ni Afis

Nafasi za kazi leo tarehe 25

Image
Nafasi za kazi Leo Tanzania Nafasi za Kazi Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Communications Officer Job at PATH, Dar es Salaam Programme Support Officer Job, Mwanza, Tanzania Consultant-Female Food Hero, Job at Oxfam, Tanzania Consultant- Baseline Survey Job at Oxfam, Tanzania Financial Management Experts Job, Arusha, Tanzania Consultant-Female Food Hero Five Years Evaluation, DSM Senior Monitoring & Evaluation Officer Job, Tanzania Program Assistant (Education) Job at UNICEF, Dar es Salaam Tembelea  STUFFZOOM  Kwa nafasi zaidi

ANGALIA PICHA PRINCE WILLIAM NA MKEWE KATE WALIVYOPAMBA MBIO ZA LONDON MARATHON

Image
Wikiendi hii yalifanyika mashindano ya riadha ya London Marathon, ambako Mtanzania Alphonce Simbu aliibuka mshindi wa tano. Prince William na mkewe Catherine Elizabeth (Kate) ni baadhi ya wageni waliohudhuria katika mashindano hayo. Katika mbio hizo Daniel Wanjiru kutoka Kenya aliibuka mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume baada ya kukimbia kwa muda wa masaa 2:05:48 na upande wa wanawake Mary Keitany naye kutoka Kenya alishinda baada ya kukimbia kwa muda wa masaa 2.17.01. Hizi ni baadhi ya picha za Prince William na mkewe Kate Middleton katika mashindano hayo.

Shehe Mkuu DSM Aibua Utata Freemason

Image
  Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salumu mwishoni mwa wiki iliyopita alizua utata katika kona mbalimbali za kijamii kufuatia kufanya dua maalumu ya kumwombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Freemason Afrika Mashariki, marehemu Sir Jayantilal Keshavji ‘Andy Chande’ (pichani). Tukio hilo lilifanyika Aprili 21, mwaka huu katika Shule ya Sekondari ya Shabani Robert na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi, akiwemo Rais Msaatafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa sanjari na wanafunzi wengine waliowahi kusoma katika shule hiyo. HABARI KAMILI Sir Andy Chande alifariki dunia, Aprili 7, mwaka huu nchini Kenya kwa maradhi ya presha na kuzikwa katika Makaburi ya Baniani, Makumbusho jijini hapa kwa kuchomwa moto. Katika enzi za uhai wake, Sir Andy Chande aliwahi kuweka wazi kuwa yeye ni mfuasi na kuhani mkuu wa Jumuiya ya Freemason, jumuiya ambayo inaaminika na baadhi ya watu kwamba iko kinyume na mafundisho ya dini za Kiislamu na

Aliyeua mwanawe kwa nyundo atakiwa kupimwa akili

Image
JAJI wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Joaquine De-Mello ameamuru mtuhumiwa wa mauaji ya mwanawe kwa kutumia nyundo na ambaye ni mchinja nguruwe, Ezekiel Magige akapimwe akili Dodoma. Magige, ambaye ni mkazi wa mji mdogo wa Sirari alifikishwa mahakamani jana kwa tuhuma za kumuua mtoto wake kwa kumpiga kwa nyundo kichwani na ubongo kusambaa. Mahakama Kuu ipo katika vikao vyake vya kikanda Tarime kwa wiki mbili na Jaji De-Mello anasaidiwa na Jaji Rose Ebrahim. Kesi zaidi ya 40 ama zitatajwa au kusikilizwa, zikihusisha makosa ya mauaji, madawa ya kulevya na ujambazi wa kutumia silaha. Wakili wa Serikali, Harry Mbogoro alidai kuwa Desemba 28, 2014 na akiwa nyumbani kwake Sirari, mtuhumiwa Magige alimpiga kwa nyundo kichwani mwanawe Julias Michael na kusababisha kifo chake papo hapo. Jaji De-Mello alisema "ninaagiza mtuhumiwa huyu Ezekeil Magige apelekwe Isanga Dodoma kupimwa akili ka

FLORA MBASHA KUOLEWA NA KUZINDUA ALBAMU MPYA SIKU MOJA

Image
Aliyekuwa Mke wa Muimbaji wa Muziki wa Injili Emmanuel Mbasha, Flora Mbasha aka Madame Flora, anatarajia kufunga ndoa na mume wake mtarajiwa Daudi Kusekwa katika bustani za hoteli ya Rock Beach jijini Mwanza. Madame Flora alisema kuwa ndoa hiyo itaambatana na uzinduzi wa albamu yake mpya inayoitwa ‘Wakati Wake’ pamoja na kitabu alichokipachika jina la ‘Siri za Flora Mbasha.’“Ndoa itafungwa asubuhi na jioni kutakuwa na sherehe ya harusi, utambulisho wa albamu yangu mpya pamoja na kitabu kipya. Watu wote wanakaribishwa, ingawa kadi zimebaki chache tu kutokana na idadi ambayo imepangwa na kamati,” alisema Flora. Chanzo Mtanzania.