Roma, Italia Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amewashangaza makahaba wa zamani 20 alipowatembelea katika ziara ya kushitukiza kwenye makazi yao yenye ulinzi mjini Roma. Papa Francis alizungumza na wanawake hao, ambao baadhi yao walisafirishwa kutoka Afrika na maeneo mengine ya Ulaya, kwa muda wa zaidi ya saa moja. Wanawake hao waliokolewa kutoka kwenye madanguro walikokuwa wametekwa na mwanamume aliyekua akiwauza kama makahaba na sasa wamepewa makazi na ulinzi katika jengo la ghorofa linalomilikiwa na kanisa katoliki katika Mji Mkuu wa Italia. Papa Francis mwenye umri wa miaka 79 amekua akirejelea mara kwa mara kwamba biashara ya kuwasafirisha binadamu “ni uhalifu dhidi ya binadamu”. Papa Francis aliketi na wanawake hao, wakiwemo wanaigeria saba, waromania sita na wanne kutoka Albania, na kusikiliza habari zao kuhusu namna walivyo lazimishwa ukahaba, ulisema utawala wa Vatican. Wengine watatu katika kundi hilo wanatoka Italia,...