UWANJA WA CCM KAMBARAGE WAJAA MAJI NA HIVYO MECHI YA KAGERA SUGAR NA SIMBA FC IMEAHIRISHWA
Mchezo wa ligi kuu Vodacoma Tanzania bara baina ya Kagera Sugar na Simba SC uliotakiwa kufanyika katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga umeahirishwa jioni hii kutokana na uwanja wa kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Shinyanga. Uongozi wa Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Shinyanga umesema hali ya hewa nzuri hivyo mchezo huo utafanyika kesho kutwa siku ya Jumatatu. Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa miguu mkoa wa Shinyanga Benister Lugola amesema mchezo utafanyika Hata hivyo pamoja na maji kujaa katika uwanja huo hususani upande wa magoli ,mashabiki wa mpira wa miguu hawajajitokeza kwa wingi hivyo hali ambayo inatajwa kuwa imechangia kwa kiasi kikubwa kuahirishwa kwa mechi hiyo ingawa timu zote zilikuwa tayari kucheza,huku timu ya Simba ikipiga kelele zaidi kwani wanatumia gharama kubwa kutokana na kwamba kesho walitakiwa kuondoka mkoani Shinyanga. Wakizungumza na Malunde1 blog Mashabiki wamelalamikia kitendo cha me...