Posts

Showing posts from January 24, 2020

Profesa Kabudi: Niliandika barua ya kujiuzulu lakini ilichanwa

Image
FRIDAY JANUARY 24 2020         Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje nchini Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuna wakati aliandika barua ya kujiuzulu lakini alinyang’anywa na ikachanwa. Mbunge huyo wa kuteuliwa na Rais ameeleza hayo leo Ijumaa Januari 24, 2020 Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na kamati ya madini ya Barrick. Kabudi anasema alichukua uamuzi wa kuandika barua hiyo baada ya mchakato wa majadiliano na wajumbe wa Barrick kuwa magumu, kwamba aliona aibu kushindwa kazi aliyotumwa. Amemtaja aliyemnyang’anya barua hiyo ambayo haikuifafanua kwa kina ni Kasmir Simbakuki. “Nilifikia hatua nikafanya dhambi ya kukata tamaa nikasema jambo hili haliwezekani, niliona ni bora aibu na fedheha hiyo niibebe lakini barua niliyoandika sikufanikiwa kuileta.” “Nilisema sijawahi kutumwa kazi na mkuu wangu wa nchi ikanishinda,” amesema Kabudi. Amesema wakati huo aliku...

Mbowe na Viongozi 8 CHADEMA sasa wanasubiria hukumu

Image
Viongozi 9 wa CHADEMA, akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wanasubiri hukumu ya kesi yao baada ya kufunga ushahidi wao wa mashahidi 15. Hata hivyo, mahakama hiyo imempa onyo mbunge wa Kawe, Halima Mdee na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya baada ya kukiuka masharti ya dhamana. Hatua hiyo imefikiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa utetezi, Peter Kibatala kueleza kuwa hawaoni haja ya kuendelea na shahidi mwingine kwa sababu ushahidi uliotolewa na mashahidi wao 15 umejitosheleza. Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 24, 2020 kwa ajili ya kufanya majumuisho ya mwisho kabla ya kutolewa hukumu.

Lulu diva ataja siri kuvaa nusu utupu

Image
K UTOKANA  na hivi karibuni kuonekana kucharuka kwa kuvaa nusu utupu, staa wa muziki wa Bongo Fleva; Lulu Abasi ‘Lulu Diva’ ameibuka na kuanika siri inayomfanya kuwa hivyo.   Akichonga na  Amani,  Lulu Diva alisema siri ya kuvaa nusu utupu ni kwamba anapenda sana kwa kuwa nguo hizo zinamfanya awe huru kila anakokwenda hata mbele za watu anakuwa jasiri zaidi. “Napenda sana kuvaa nguo fupi zinazoonesha jinsi nilivyoumbika kwa kuwa nakuwa huru zaidi, sijali mtu mwingine ataizungumziaje maana watu wamezoea kutoa povu kwa kila kitu kiwe kibaya au kizuri kwa hiyo sijali wala nini, nitaendelea kuvaa ninachokipenda ili mradi niwe huru,” alisema Lulu Diva