Posts

Showing posts from March 27, 2018

Mbowe, Mashinji, Mnyika na Wengine Wawekwa Mahabusu Sentro

Image
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe na baadhi ya viongozi wengine waandamizi wa chama hicho akiwepo Katibu Mkuu Dkt Vincent Mashinji, John Mnyika, Salum Mwalimu na Ester Matiko wamewekwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha polisi Dar es Salaam. Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha hilo na kusema kuwa viongozi hao wamewekwa mahabusu leo Machi 27, 2018 baada ya kuripoti Kituo Kikuu Cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao. “Viongozi Wakuu wa Chama pamoja na wabunge waliokuwa wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao, wamewekwa mahabusu. Polisi hawajaeleza sababu ya kufanya hivyo. Mawakili wetu wanashughulikia. Tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi,” alisema Makene.

Maua Sama afunguka mwaka wa kuolewa

Image
Maua Sama.   MKALI mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Maua Sama kwa mara ya kwanza ametaja mwaka wa kuolewa kuwa mambo yakienda sawa mwaka huu unaweza kuwa wake. Awali zilienea tetesi kuwa, staa huyo anayebamba na Ngoma ya Nakuelewa amechumbiwa na mpenzi wake ambaye ni Mzungu lakini mwenyewe ameibuka na kukanusha. “Nilishangaa kwa kweli hilo suala la kuchumbiwa na Mzungu kwani halikuwa la kweli, kuhusu kuolewa nimekuwa nikisikia kwa mashabiki sana, ndoa ni mipango, maombi yao yanaweza kunifanya nikatimiza hilo na inawezekana hata mwaka usiishe,” alisema Maua.

Wapiga picha za utupu wadakwa na Jeshi la Polisi

Image
Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linawashikilia watu 6 akiwemo Mabula Mabula mkazi wa mji mpya kwa tuhuma za kujifanya askari na kuwakamata wanawake nyakati za usiku, kuwapora mali, kuwafanyia vitendo vya kikatili kuwalawiti na kuwapiga picha za utupu. Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei na kusema kukamatwa kwa mtuhumiwa Mabula ni kufuatia matukio kadhaa ya aina hiyo yaliyo ripotiwa kutokea katika maeneo tofauti ya mji huo. Kamanda Mtei amesema baada ya kupata taarifa, jeshi hilo kwa kushirikiana na timu ya wataalam wa makosa ya mitandao pamoja na Kikosi cha kupambana na ujambazi wakafanikisha kupatikana kwake ambaye baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kuhusika matukio hayo na kudai anafanya hivyo kwa lengo la kujipatia fedha. Kwa upande mwingine, Jeshi hilo linawashikilia watu watatu ambao ni vinara wa matukio ya utapeli pamoja na wizi kwa njia ya mtandao wakiwa na simu 9 pamoja na line 57 za mitandao mbalimbali zinazotumika kufa

BREAKING NEWS:JPM Awasimaisha Kazi Wakurugenzi Halmashauri Kigoma Ujiji, Handeni

Image
IKULU: Rais Magufuli amewasimamisha kazi Wakurugenzi wa Halmashauri za Kigoma Ujiji na Pangani baada ya kuandikiwa hati chafu kwenye Vitabu vya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyowasilishwa leo. “Kuna Wilaya mbili, Halmashauri Mbili zina hati chafu, Mimi nafikiri Kigoma Ujiji na Pangani, Mimi nafikiri saa nyingine tuchukue hatua kwa vile Waziri wa TAMISEMI upo hapa WAKURUGENZI wa Wilaya hizo WASIMAMISHWE kazi leo” -Rais Magufuli

MAJIBU YA DAKTARI SIMBA BAADA YA MKUDE KUUMIA JANA

Image
Kiungo mchezaji wa Simba, Jonas Mkude , aliumia jana wakati kikosi hicho kikijiandaa na mazoezi kuelekea mchezo ujao wa ligi dhidi ya Njombe. Mkude aliumia wakati akiwania mpira na kiungo mshambuliaji, Mzamiru Yassin na kuepelekea kuanguka chini kisha kutolewa nje ya Uwanja wa Boko Vetarani. Kufuatia kuumia huko, kwa mujibu wa Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, Daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe , alisema Mkude hajapata maumivu makali, na anaweza akarejea baada ya siku mbili mpaka tatu. Wakati Simba inajiandaa kuivaa Njombe Mji, Aprili 3 2018 , kumekuwa na hofu kubwa kwa mashabiki kama ataweza kurejea mapema, japo majibu ya Daktrari yameeleza hatachukua muda mrefu. Na George Mganga.

Breaking: Abdul Nondo Asimamishwa Masomo Chuo Kikuu

Image
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) , Profesa William Anangisye, amemsimamisha masomo Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo hadi kesi yake ya kutoa taarifa za uongo mitandaoni na kudanganya kutekwa itakapomalizika. Nondo alipewa dhamana na mahakama ya Iringa, jana Jumatatu,Machi 2018 baada ya kusota rumande kwa wiki kadhaa. TAARIFA YA CHUO KIKUU DAR ES SALAAM