Posts

Showing posts from January 8, 2014

WASANII WENYE HOFU YA KIFO HAWA HAPA

Image
HOFU ya kifo imetawala kwa mastaa Bongo ikiwa ni siku chache baada ya gazeti hili toleo la Jumamosi iliyopita kutoka na habari ya utabiri wa Hussein Yahaya, ikieleza kuwa mwaka huu vifo zaidi vitaendelea kwa wasanii wa filamu, muziki, waandishi wa habari, viongozi wa dini na wanasiasa. Aunt Ezekiel. Risasi Mchanganyiko limepata kuzungumza na baadhi ya wasanii wa sanaa mbalimbali Bongo na kueleza maoni yao kuhusiana na utabiri huo. Wa kwanza kuzungumza alikuwa ni Single Mtambalike ‘Richie’ aliye msanii wa filamu ambaye alisema: “Namwamini Mungu kwa asilimia zote, hata kama kitatokea kifo mbele yetu nina imani kitakuwa na sababu kama ugonjwa na kadhalika, siyo ghafla." SHAMSA FORD "Unajua ibada ndiyo kitu cha kwanza kutuokoa, mimi natoa rai kwa wenzangu wakumbuke kuomba kila mtu kwa imani yake tutashinda tu." AUNT EZEKIEL "Haya yanayotokea inabidi tujifunze na yaliyopita, mimi kwangu naona kama changamoto nyingine. Naahidi kumtukuza Mungu il...

MKONO ATOBOA SIRI ZA ZITTO

Image
Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono ametoa ufafanuzi juu ya uhusiano wake na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe. Hatua hiyo ya Mkono imekuja baada ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kumtuhumu kuwa aliwahi kumpa Zitto magari mawili. Katika taarifa yake aliyoitoa jana, Mkono alisema kuna magari mawili yanayohusishwa na Zitto na kuyataja kuwa ni Toyota Land Cruiser na Nissan Patrol. "Sijawahi kumpatia Zitto magari, isipokuwa kuhusu hiyo Land Cruiser, nilitoa msaada wa kuwanusuru Zitto na Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe), kule Tarime kwenye msiba wa marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Chadema), kwani walikuwa wakitishiwa kupigwa." Alisema alitoa gari hilo lililokuwa na Bendera ya Bunge liwachukue Mbowe na Zitto na kuwapeleka Mwanza... "Walipofika Mwanza, Zitto aliwasiliana na mimi kuhusu ununuzi wa gari hilo na kupitia wakala wangu nilimuuzia," alisema Mkono. Kuhusu Nissan Pa...

HIVI NDIVYO MSANII MEZ B ALIVYOUMIZWA USONI NA KISU NA MTU ASIYEFAHAMIKA JIONEE

Image
Taarifa za msanii Mez B kushambuliwa na mtu asiemfahamu wala kuwa na ugomvi nae usiku wa Jumamosi akiwa maeneo ya Sinza ni miongoni mwa stori zilizosambaa sana toka jana. Mez B kwenye interview fupi na millardayo.com amesema amepata majeraha mengi maeneo ya usoni na anasema kwamba kuna kisu alikikwepa kikielekezwa shingoni wakati aliporushiwa visu mbele ya Mabaunsa wa sehemu ya burudani Sinza waliokua wakishuhudia bila kutoa msaada wowote. Mez B tayari ameshaifikisha hii ishu kwenye vyombo vya sheria ili kila kitu kikae kwenye mstari kuhusu mtu huyu aliemshambulia ambae Mez anadai alimkuta mahali anasubiria kufungiwa chips zake ndio akaanza kutukana watu mbalimbali ikiwemo Serikali na Mez B mwenyewe. Baada ya hapo wakati Mezi akiondoka, baunsa mmoja kwenye eneo hilo alimwita na kumwambia haiwezekani huyu jamaa akutukane hivihivi hebu njoo tumuulize, tofauti na alivyotarajia… Mez anasema yule Baunsa ndio alimfata yule mchoma visu na kumwambi...

ANGALIA PICHA YA UNYAMA...KIKONGWE ACHINJWA KAMA KUKU HUKO KAHAMA,,,,UCHAWI WAHUSISHWA..!

Image
I  Mwanamke mmoja Alifahamika kwa jina la Milembe Jengamalulu anayekadiriwa kuwa na  umri wa miaka 50-55, mkazi wa Ulowa no 4 wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga umri wa miaka 50-55, amefariki dunia baada ya kuchinjwa na watu ambao mpaka sasa hawajajulikani. MWILI wa Marehemu Milembe Jengamalulu ukiwa eneo la tukioKwa mujibu wa majirani tukio hilo limetokea katika mkesha wa mwaka mpya majira ya saa moja usiku, nyumbani kwake maeneo ya Ulowa no 4 ambapo kikongwe huyo alikuwa anaishi na mtoto wake wa kiume. Wameeleza kuwa Wakati tukio hilo likitokea, mtoto wake wa kiume ambaye hakutajwa jina lake (miaka 34-40) alikuwa ameenda kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya akiwa na mkewe maeneo ya Ulowa no 5, na wote walirudi nyumbani majira ya saa 10 na usiku ndipo walikuta mwili wa marehemu Milembe Jengamalulu. Baada ya kuukuta mwili huo ukiwa nje ya nyumba huku ukiwa umetapakaa damu nyingi, huku ukionesha kuwa amechijwa kwa kutumia panga na shoka, walitoa...

Shukuru kwa kupewa afya nzuri, tazama ugonjwa wa ajabu unavyomtafuna mtu huyu...

Image
Wakati mwingine binadamu huwa tunajisahau kumshukuru Mungu kwa afya nzuri aliyotupa bila kujua kuwa wapo watu duniani wanaoteseka mno. Mwanaume huyu wa nchini Indonesia ambaye  mwili wake umefunikwa na upele mkubwa ameiomba dunia imsaidie kumponya tatizo lake ambalo sasa limesababishwa ashindwe kuona vizuri baada ya madude hayo kufunika macho yake. Slamet, anayetokea East Java, anaaminika kuwa na ugonjwa uitwao neurofibromatosis. Kwa mujibu wa kaka yake, Suwadi, ndugu yake huyo mwenye miaka 59 aliondolewa kitu kama jipu kwenye kiuno chake mwaka 1991. Lakini miezi sita baadaye vipele vingine vikaanza kutoka usoni na kwenye mwili wake.   Miaka kadhaa baadaye hali hiyo imekuwa isiyovumilika kwakuwa Slamet husikia maumivu mwilini muda wote. Majipu hayo kwa sasa yamekuwa mengi kiasi cha kuziba pua zake na kumfanya apumue kwa tabu.