Kigwangalla: “Walipanga Kuniangamiza, Walitaka Nitumbuliwe”
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangalla, ameeleza kuwa kwa sasa anaishi kwa hofu na tahadhali kubwa juu ya uhai wake kutokana na kuwepo kwa kundi la watu wanaomuwinda wakitaka kumuangamiza huku wengine wakimfanyia mipango ya kumuharibia ili atumbuliwe uwaziri. Kupitia akaunti yake ya instagram Kigwangala ameweka wazi kuwa hata alivyopata ajali aliwekewa ulinzi mkali wodini ili wabaya wake wasiweze kummalizia kwa namna yoyote. Kupitia instagram yake ameandika hivi; Sikusudii kufanya press conference. Watu wengi wamenishauri niishie hapa. Team yangu imefanya kazi nzuri, imenipa uthibitisho wa majina ya wanaotaka nichafuliwe ili niondolewe uwaziri. Bahati mbaya hakuna cha kunichafua nacho, wanapika hadithi za kitoto na kurudia tu. Walidhani ningekaidi maelekezo ya Mhe. Rais juu ya mgogoro wa ndani ya Wizara yetu ili Rais achukie aniondoe, wakakwama. Sikukaidi. Wakaona wafanye mwendelezo kupitia gazeti, sijataka kujibishana nalo, tutakutana mahakamani ambapo m...